Na Joseph Ngilisho ARUSHA
WATU wanne wa familia moja wakazi wa Ngulelo jijini Arusha wamenusurika kuuawa na kujeruhiwa vibaya wananchi wenye hasira kali wilayani Mbulu wakidhu ni watekaji wa watoto baada ya kuharibikiwa na gari wakitoka harusini.
Tukio hilo la kustaajabisha limetokea katika kijiji cha MÀQANG,Hydom wilayani humo baada ya wananchi hao wakiongozwa na viongozi wa eneo hilo kuwazingira na kuanza kuwashambulia kwa mawe na mapanga na kisha kuteketeza kwa moto gari walilokuwa wakilitumia baada ya mmoja wa majeruhi kuonekana akimpatia pipi mtoto wa wananchi hao na kuhisi wanataka kumteka.
Akisimulia mkasa wa tukio hilo mmoja ya majeruhi hao,Neema Kilaye ambaye amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Arumeru, TENGERU, alisema kuwa siku ya tukio,Agosti 24 mwaka huu,walitoka katika kijiji cha Kidarafa kufanyakazi ya kupika chakula kwenye harusi na walipofika katika kijiji hicho cha Maqang waliharibikiwa na gari na kuamua kupumzika .
"Siku ya jumamosi majira ya saa 9 alasiri gari letu aina ya Raum liliharibika tairi tuliamua kushuka na kwenda eneo la Lenye duka kutafuta mahitaji ikiwemo kuchaji simu tukiwa hapo tuliona wananchi hao wakilizunguka gari letu na baadaye walitufuata huku wakiongea kwa lugha ya kwao ya Kimbulu na kuanza kutushambulia"
Neema ambaye alijeruhiwa sehemu za tumbo na mbavu alisema kabla ya wananchi hao kuteketeza gari lao na kuwashambulia walipora fedha ,simu,nyama ,mchele ,maharage na vitu vyote vilivyokuwa kwenye gari .
Majeruhi mwingine Arnold Jackson ambaye amelazwa katika hospitali hiyo alidai kunyolewa rasta zake kwa panga na kisha kushambuliwa kichwani na wananchi hao waliokuwa zaidi ya 100 na alishukuru polisi waliofika eneo la tukio na kufanikiwa kuwaokoa wakiwa taabani.
Wengine waliojeruhiwa na wapo katika hali mbaya katika hospitali ya Rufaa ya KCMC mkoani Kilimanjaro ni ,Mina Sekibaha na Antony Francis ambaye alivunjwa taya kwa kupigwa na jiwe.
Majeruhi hao wameiomba serikali kuwachukulia hatua wananchi hao akiwemo diwani wao ambao walijichukulia sheria mkononi kwa kuwashambuli bila hatia yoyote .
Ends. ...
0 Comments