VIONGOZI WA DINI WAJITOSA KUHAMASISHA UTALII NCHINI,WAVUTIWA NA KASI YA RAIS SAMIA YA KUTANGAZA UTALII KUPITIA FILAMU YA ROYAL TOUR

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Viongozi wa dini ya Kiislamu Mkoa wa Arusha,wameamua kuunga mkono  jitihada za serikali katika kuhamasisha utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio mbalimbali ikiwa ni hatua moja wapo ya kuvitangaza vivutio vya  utalii nchini.


Msemaji wa taasisi ya dini ya kiislamu ya Twarika  Sheikh Haruna Husein alimpongeza rais Samia Suluhu kwa kuwa mzalendo wa kwanza akiwa madarakani kucheza filamu ya Royal Tour yenye lengo la kutangaza vivutio na kuhamasisha utalii .


Alisema baada ya filamu hiyo ya Royal Tour, watalii kutoka mataifa mbalimbali walihamasika na kumiminika nchini kujionea vivutio hivyo na wao kama viongozi wa dini wameonelea ni wakati mwafaka kumuunga mkono juhudi za rais Samia kwa kutembelea hifadhi na kutangaza 
Vivutio hivyo.
"Kama Rais Samia aliamua kujitolea kutengeneza filamu ya kutangaza utalii wetu sisi ninani nani tushindwe kumuunga mkono ,ndio maana sisi kama viongozi wa dini tumechukua jukumu la kutangaza vivutio vyetu na tutazindua kauli mbiu yetu yenye kuelezea nini kimetusukuma kutembelea vivutio na kuhamasisha utalii wetu "

Sheikh Haruna alilipongeza shirika la hifadhi za Taifa Tanapa chini ya kamishna wa uhifadhi Juma Kuji ,kwa kuweka mazingira mazuri ambayo yamerahisisha kwa kila mtanzania kuweza kutembelea hifadhi hizo na kujifunza.

Katika hatua nyingine Sheikh Haruna alitoa rai kwa viongozi wa dini hiyo kushikamana kwa pamoja na kuwaunganisha waislamu ili kuondoa makundi yanayoleta mgawanyiko.

Naye kiongozi mwingine wa dini hiyo, kutoka  taasisi ya zawiya ,alisema ziara hiyo ya kutembelea vivutio vya utalii wanatarajia kuifanya agosti 17 mwala huu katika hifadhi ya Tarangire ili kujionea vivutio na kuvitangaza .

"Tumeamua kumuunga mkono kwa vitendo rais Samia kwa kutembelea hifadhi zetu kwani  ni jukumu letu kama viongozi wa dini kuyaeleza mema yote tutakayoyaona kwenye hifadhi zetu"

Ends..







Post a Comment

0 Comments