VIJANA WANASWA CHUMBANI WAKIFANYA MAPENZI YA JINSIA MOJA KWA ZAMU MCHANA KWEUPE,MIGUNO YAWASHTUA MAJIRANI ,MWENYEKITI WA MTAA AKANUSHA KUWATOROSHA "WAPO POLISI"

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

 

Sakata la Vijana wawili wanaoshikiliwa na polisi kukutwa wakifanya mapenzi ya jinsia moja katika chumba kimoja mtaa wa Olmokea ,kata ya Sinoni jijini Arusha ,limechukua sura mpya kufuatia wananchi wa mtaa huo kufanya operesheni  ya nyumba kwa nyumba kuwasaka vijana wanaojihusisha na tabia hiyo .



Wakiongea na waandishi wa habari wananchi hao walimpongeza Mwenyekiti  wa mtaa huo ,Abdalah Mgongo kwa kupinga ushoga na kufanikisha kuwakamata vijana hao na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria na kuwataka wananchi kuwafichua vijana wenye dariri zinazohusiana na ushoga ili kukwepa kuambukiza watoto tabia hiyo.

Wananchi hao, Salimu Mbega,Hawa Juma Ally na   Sophia Songa walisema kuwa vitendo vya ushoga vinapaswa kupingwa kwa nguvu zote na kumpongeza  Mwenyekiti wao kwa kuwa mstari wa mbele kulaani vitendo hivyo huku wakisisitiza kuwa  wanaompaka matope Mwenyekiti wao kuwa aliwatorosha watuhumiwa na baadaye kuwaachia wanania ya ovu ya kumchafua !

"Wanaozusha kwamba Mwenyekiti aliwatorosha wahusika sio kweli watuhumiwa walikamatwa na walipelekwa sehemu husika"


Akiongelea tukio hilo Mwenyekiti wa mtaa huo,Abdalah Mgongo alisema hakubaliani na tabia ya ushoga katika mtaa wake ila alikiri kwamba  tukio la vijana hao limewafedhehesha na wapo katika hatua ya kufanya msako wa nyumba kwa nyumba kubaini vijana wanaojihusisha na  mapenzi ya jinsia moja  na kuchukua hatua.


Hata hivyo Mgongo alikamusha kuwatorosha vijana hao na kuuchia kama ambavyo baadhi ya watu  wachache wanavyozusha kwa lengo la kumchafua


Aidha alisema siku ya tukio alipata taarifa ya kuwepo kwa vijana wawili waliokuwa wamejifungia katika chumba kimoja majira ya saa saba mchana wakifanya vitendo vya ushoga kwa kuingiliana kwa zamu na alipofika na kuingia ndani ya chumba hicho aliwakuta na kuwapeleka kituo cha polisi kwa ajili ya maelezo ya kina na  baada ya kuhojiwa walikiri kujihusisha na ushoga kinyume cha sheria.


Alisema siku ya tukio wananchi walizingira nyumba hiyo na kuwafungia ndani ya chumba hicho baada ya mmoja ya wananchi hao kusikia miguno ya kimahaba na kuwaita wananchi wengine ambao walijikusanya kwa lengo la kutaka kuwachomea ndani ila Mwenyekiti huyo aliwahi kufika na  kufanikisha kuwaokoa.


Vijana hao ambao majina yao yanahifadhiwa wanaumri wa miaka 22 na 23 na mmoja wapo hufanya kazi ya kuuza vyuma chakavu na mkazi wa mtaa huo huku mwingine akidaiwa kuishi eneo la mianzini Jijini hapa.


Kamanda wa polisi Mkoani Arusha ,Justine Masejo hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo ila taarifa zinasema kwamba watuhumiwa wanashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya uchunguzi ili kubaini mtandao zaidi wa mapenzi ya jinsia moja.


Ends. 


Post a Comment

0 Comments