UNGA WA KENMILL (Hakuna Matata) HABARI YA MJINI ,WAWA KIVUTIO MAONESHO YA NANE NANENANE ARUSHA, WANANCHI WAGOMBEA NI BAADA YA KUGUNDUA UNA KIRUTUBISHO

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Kampuni ya Kijenge Animal Products Limited ya jijini Arusha inayozalisha  vyakula vya binadamu na mifugo, imepata mafanikio makubwa baada ya  kufanikiwa kuzalisha unga bora wa lishe wa Kenmill  wenye kirutubisho na kuhakikisha jamii inapata lishe bora ili kuwa na nguvu kazi yenye Tija kwa taifa .


Mmoja ya wauzaji wa unga huo wa KENMILL katika Maonesho hayo ya nane nane Njiro jijini Arusha,kutoka kampuni ya kijenge Animal, Mohamed Imamu alisema kuwa bidhaa hiyo maarufu kwa jina la Hakuna Matata,inazalishwa katika ubora wa hali ya juu ndio maana imekuwa kimbilio la walaji na wamefanikiwa kuteka soko la unga bora wa ugali hapa nchini na nchi jirani ya Kenya.

Alisema kuwa kampuni ya Kijenge Animal Products Limited ina mashine bora yenye uwezo wa kuchambua uchafu na kubaki mahindi peke na pia wanachanganya na virutubisho ambavyo vinaongeza nguvu kwa mlaji na makuzi kwa watoto.

Alisema wanazalisha unga wa kilo Moja ,Tano na Kilo 25 na pia wanatoa huduma ya kumpeleke mteja popote alipo kutokana mahitaji yake.

"Bila shaka umeona wateja walivyotuzunguka hapa hii ni ishara kwamba unga wetu wa Kenmill unakubalika sana na tunasoko maeneo mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi unga wetu ni bora sana kwa sababu unazalishwa na mashine za kisasa "





Miongoni mwa wateja wa unga wa Kenmill ni Neema Mroso ambaye alisema kuwa amekuwa mteja wa muda mrefu wa unga huo kwa sababu ugali wake ukipikwa ni mtamu na hauna uchafu na unaweza kula hata bila mboga.

"Mimi ni mteja wa muda mrefu sana wa unga wa Kenmill kwa kweli ni unga mzuri sana unavirutubisho ukila hutatanani kuacha unaweza kula hata bila mboga"

Kiwanda cha Kijenge Animal Products Limited kinazalisha pia Mafuta ya kupikia  Unga lishe,Mkaa Mbadala na machinjio ya Kuku nankinapatikana eneo la Njiro Jijini Arusha.







Ends...












Post a Comment

0 Comments