TCD YAANZISHA JUKWAA LA MAJADILIANO ARUMERU, LENGO NI KUFUTA SIASA ZENYE CHUKI,DEUS KIBAMBA ATOA NENO AIPONGEZA TCD KWA KULETA MAPINDUZI YA KISIASA

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Kituo cha Demokrasia Tanzania  (TCD),kimeanzisha  jukwaa la Majadiliano ya vyama vya siasa wilayani Arumeru kwa lengo la kuimarisha , kudumisha na kulinda Demokrasia hapa nchini ili kuondoa changamoto za kisiasa zinazosababisha uvunjifu wa amani hasa kipindi cha uchaguzi .


Mradi huo wa kuunda jukwaa la Majadiliano umefadhiliwa na ubalozi wa Ayalend nchini Tanzania ambapo vyama vitano vya siasa nchini,CCM,CHADEMA, ACT-WAZALENDO,NCCR -MAGEUZI NA CUF vinashiriki Mpango huo.


Afisa Programu wa TCD ,Likele Shungu alibainisha hayo jijini Arusha,wakati alipokutana na viongozi wa siasa ngazi ya wilaya hiyo,jumuiya za vijana na wanawake ,katika kikao kilicholenga kuwaleta pamoja wanasiasa wa vyama vitano vya siasa na kuunda jukwaa la Majadiliano likiwahusisha wanasiasa hao na watendaji wa serikali .


Alisema jukwaa la Majadiliano litasaidia  kuwakutanisha wanasiasa  wakiwa katika chombo kimoja cha majadiliano chenye kuleta utulivu na kudumisha demokrasia pamoja na kutatua changamoto za kisiasa kabla hazijaleta uvumilivu wa amani.


Alisema jukwaa hilo limeundwa kwa mujibu wa sheria huku Noel Severe kutoka CCM akichaguliwa kuwa mwenyekiti wa jukwaa hilo  na Katibu wake Arapha Mohamed  kutoka CUF,ikiwa ni majukwaa 18 ambayo yameshaundwa katika wilaya mbalimbali nchini.

"Hadi sasa ni majukwaa 18 yameshaundwa katika wilaya 16 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2021 na yameoneasha mafanikio makubwa kwa kupunguza changamoto za kiasiasa  na tumeanza hasa maeneo yenye changamoto za kisiasa".

"Moja ya majukumu ya  jukwaa hilo ni kutatua changamoto za kisiasa zinazojitokeza kabla ya kuleta athari na maeneo mengi jukwaa hili limekuwa na mafanikio makubwa "Alisema Shungu


Naye mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini, Mwalimu Deus Kibamba ,alisema kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)kimeonesha mafanikio makubwa katika kuleta maridhiano katika duru za kisiasa na kupunguza siasa za kukasimiana zilizoshamiri kipindi cha nyuma.


Alisema uanishwani  jukwaa la Majadiliano ni hatua nzuri kwa siasa za Tanzania na nijambo linalopaswa kuigwa na nchi zingine na hakutakuwa na ulazima wa kufikishana kwenye vyombo vya sheria na kwamba mambo ya kisiasa lazima yamalizike kwenye meza ya mazungumzo .


"Jukwaa hilo kwa sasa linaundwa na vyama vitano vya siasa hapa nchini CCM,CHADEMA ,ACT-WAZALENDO ,NCCR-MAGEUZI na CUF  tungependa vyama vyote vya siasa vishirikishwa katika jukwaa hili na hii itasaidia sana kuondoa misuguano inayosababisha watu kupigana na mpaka kusababisha vifo"Alisema Kibamba.

                         


 Naye Mwenyekiti wa jukwaa hilo (TCD), Noel Severe ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arumeru, alisema atahakikisha jukwaa hilo linatenda haki katika maamuzi yake bila kupendelea ama kukandamiza chama chochote cha siasa.

"Baada ya kuchaguliwa Nitahakikisha nasimamia R4 za Rais Samia kuhakikisha nadumisha Amani na vyama vyote vya asiasa vinaenda pamoja nankutatua changamoto zote za kisiasa "


Mmoja wa washiriki wa jukwaa hilo Arapha Mohamed aliipongeza serikali kwa kuruhusu Demokrasia na kumwomba rais Samia kusimamia haki kwa vyama vyote vya siasa wakati wa uchaguzi jambo litakalosaida kuondoa udanganyifu na vurugu za kisiasa.


Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa walipongeza hatua ya kituo hicho cha TCD kuibua jukwaa hilo la majadiliano wakidai litaleta mapinduzi ya kisiasa nchini ila walidai kwamba katika vikao vya uundwaji wa majukwaa hayo  ni muhimu viongozi wa wilaya kama mkuu wa wilaya  na wakuu wa polisi wa wilaya wawepo  ili kujibu hoja kwani baadhi yao  wanawatuhumu kutumika na chama tawala kudhoofisha vyama vya upinzani nchini.







Ends.. 
















Post a Comment

0 Comments