TAZAMA VIBE LA MASHABIKI WA YANGA ARUSHA, WAKABIDHI MISAADA KIBAO HOSPITAL YA MT MERU ,WATUMA SALAMA KWA SIMBA GOLI NANE ZINAWAHUSU AGOSTI 8 MWAKA HUU


Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Katika kuelelea kilele cha siku ya wananchi  mashabiki na wapenzi wa YangaTawi la Arusha  wamefanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali katika hospitali ya Rufaa Mont Meru huku wakitamba kuibuka na ushindi wa gori 8 bila dhidi ya watanu wao Simba, agost 8 mwaka huu.

Akiongea na vyombo vya habari katika hospitali ya Mt Meru ,Mratibu wa Tawi la Yanga Mkoa wa Arusha,James Rugangira alisema msaada huo ni utaratibu wao wa kila mwaka kujitoa na kusaidia jamii ni ikiwa ni hatua yao kuhamasisha michezo hapa nchini.

"Msaada huu tumeutoa ikiwa ni wajibu wetu kama wanamichezo kusaidia jamii hasa kipindi hiki tunapoelekea kilele cha wananchi huu ni utaratibu wetu wa kila mwaka na kupitia sisi viongozi wa matawi tumewakilisha idadi kubwa ya mashabiki na wapenzi wa yanga Arusha"

Aidha mashabiki wa timu hiyo ya Yanga wamejigamba kuibuka na ushindi  dhidi ya wapinzani wao simba watakapokutana kwenye mchezo wa ngao ya jamii utakaopigwa agosti nane mwaka huu.

Mashabiki hao zaidi 300 wanatarajiwa kuondoka leo jijini Arusha kuelekea jijini Dar kwa ajili ya kilele cha Wananchi hapo agost 4 mwaka huu .










Ends..






Post a Comment

0 Comments