By Ngilisho Tv
MTOTO Maliki Hashimu, mkazi wa Goba Jijini Dar es Salaam, aliyekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutokana na majeraha makubwa aliyopata baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mfanyakazi wa ndani ‘house girl’, ameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya madaktari kujiridhisha na hali yake.
Kitu hicho chenye ncha kali kilitenganisha njia ya hewa chini ya sanduku la sauti na kusababisha ashindwe kupumua, kuongea, kupata maumivu na kupoteza damu nyingi
Mama mzazi wa Malik
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatano kuhusu maendeleo ya kitabibu ya mtoto huyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk. Rachel Mhavile amesema watalaam wa hospitali wamejiridhisha kulingana na huduma alizopata mtoto huyo tangu alipopokelewa tarehe 15 Julai mwaka huu kuwa sasa yupo salama na ataenda nyumbani ili kuendelea na shule na maisha yake ya kawaida huku hospitali ikiahidi kufuatilia kwa karibu maendeleo yake.
Naye Daktari Bingwa wa Tiba na Magonjwa ya Dharura, Dk. Juma Mfinanga amesema baada ya mtoto huyo kupokelewa akiwa na hali mbaya kutokana na majeraha aliyopata walihakikisha anapata huduma ya kwanza ya kurejesha hali ya upumuaji, kupata damu na badaye kuita timu husika ya wabobezi wa upasuaji wa shingo, pua, koo na masikio.
0 Comments