By Ngilisho Tv-Hai.
Watu wawili wamefariki
dunia, akiwamo Mchungaji
wa Usharika wa Kimashuku,
Dayosisi ya Kaskazini ya
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Kantate
Munis (42) baada ya gari
walilokuwa wakisafiria
kugongana na basi kubwa la
abiria.
Akizungumza leo Jumatatu Agosti 5, 2024,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, Simon Maigwa
amesema ajali hiyo ilitokea
jana Jumapili Agosti 4,
2024 eneo la Kimashuku
Kata ya Mnadani wilayani
Hai, Mkoa wa Kilimanjaro,
wakati gari ya mchungaji
huyo akikatiza barabara
upande wa kulia kuingia
kanisani kwake.
Kamanda Maigwa amewataja
waliofariki dunia mbali ya
Mchungaji Munis ni Laban
Kweka (50) ambaye ni mzee
wa kanisa hilo, wote walifia
eneo la ajali.
"Ni kweli jana kulitokea ajali
iliyohusisha gari dogo na
basi la abiria lililokuwa
likitokea Dodoma kuja Moshi
mjini, lilipofika eneo la
Kimashuku, Mailisita
liligongana na gari dogo na
kusababisha watu wawili
kufariki dunia na majeruhi,"
amesema kamanda huyo.
Mwananchi imezungumza na
msaidizi wa Mkuu wa Jimbo
la Hai, Dayosisi ya Kaskazini
уа КККТ, Mchungaji
Dominick Mushi aliyesema
ajali hiyo imetokea wakati
mchungaji huyo akiingia
usharikani Kimashuku.
Amesema Mchungaji Munis
alikuwa akitokea kwenye
uimbaji wa kikanda
Bomang'ombe wilayani Hai
na alipofika eneo la
Kimashuku ndipo alipopata
ajali hiyo.
"Jana tulikuwa kwenye
uimbaji wa kikanda,
tulipomaliza ndipo
mchungaji akatoka kurudi
usharikani ambako ndipo
anaishi nyumba za usharika
na wakati amefika
Kimashuku akiingia
usharikani akapata ajali.
"Mchungaji alikuwa anaingia
usharikani Kimashuku na
basi lilikuwa linayapita
magari mengine ndipo
likaigonga gari ya mchungaji
kwa ubavuni na kusereresha
hadi kwenye miti," amesema
na kuongeza kuwa gari hilo
lilikuwa na watu saba,
wengine watano wamepata
majeraha.
Mushi amesema majeruhi
hao ambao ni mama na
watoto wake wamepelekwa
Hospitali ya Mawenzi na
wengine wawili wamelazwa
Hospitali ya Wilaya ya Hai
wakiendelea na matibabu.
Mwili wa Mchungaji Munis
umehifadhiwa Hospitali ya
Rufaa ya KCMC, huku wa
mzee wa Kanisa
ukihifadhiwa katika
Hospitali ya Wilaya ya Hai
kusubiri taratibu za maziko.
Endelea kufuatilia
Mwananchi.
0 Comments