MASIKINI RPC HUYU MDOMO WA MPONZA AONDOLEWA CHAP,SASA KUSOMA MAGAZETI ,WANANCHI MANYARA WAMLILIA SACP KATABAZI

By Ngilisho Tv


Jeshi la Polisi limesema kauli aliyoitoa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Theopista Mallya kuhusu binti aliyefanyiwa ukatili kuwa ‘alikuwa kama anajiuza’ si msimamo wa Jeshi la Polisi

SACP Theopista Mally

"Kilichobainika vijana hao hawakutumwa na askari, walikuwa kama walevi na wavuta bangi tu, lakini yule dada alikuwa kama anajiuza ‘kahaba’.”Alisema RPC Mally

Kauli hiyo imekuja baada ya RPC kuzungumza na chombo cha Habari hapa nchini kwa njia ya simu ambapo aliulizwa ikiwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na swali lingine aliloulizwa ni madai ya binti huyo kujiuza ambapo majibu ya kamanda huyo alisema hata kama ni hivyo hangestahili kutendewa hivyo.


Aidha, Jeshi hilo limechukizwa na kauli hiyo na limesema kuwa wakati wa uchunguzi wa tukio hilo , Mkuu wa Jeshi la Polisi amemhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Theopista Mallya kwenda Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP George Katabazi.


WAKATI huo huo WANANCHI na wakazi wa Mkoa wa Manyara,wameingiwa na huzuni kubwa kufuatia kuhamishwa kwa aliyekuwa RPC Mkoani humo,SACP George Katabazi aliyehamia Mkoani Dodoma ,wakidai kuwa alilifanya jeshi hilo kuwa rafiki na ushirikiano nzuri na WANANCHI.

SACP Katabazi 

WANANCHI hao walidai kupoteza mtu makini anayejali utu na sasa wameingiwa na majonzi kwa kutolewa kwa kamanda wao.


"Unajua Kamanda Katabazi alikuwa Mwema sana ulikuwa ukimpigia simu hata usiku wa manane anakusaidia alilifanya jeshi la polisi kuwa na mahusiano na ushirikiano mzuri na jamii sijui kama tutapata RPC kama huyo" alisema Jamal Matua mkazi wa Babati


Ends


Endss

Post a Comment

0 Comments