Na Joseph Ngilisho ,MOSHI
Kesi ya Mirathi iliyodumu kwa muda mrefu wa miaka 22 imeshindwa kuendelea katika mahakama kuu ya Moshi Mkoani Kilimanjaro baada ya jalada muhimu lenye mwenendo wa kesi hiyo kupotea katika mazingira ya utata mahakamani
Kesi hiyo imekuja leo agosti 13,mwaka ikiwa ni hatua ya kutafuta haki kwa wanufaika baada ya kifo cha aliyekuwa mfanyabiashara mkubwa mjini Moshi marehemu Paul Kyauka Njau aliyefariki mwaka mwaka 2002 na kuacha watoto zaidi ya 20,mali nyingi yakiwemo Magari Majumba ,Mashamba na fedha benki.
Jaji wa mahakama hiyo, Safina Simfukwe amebainika hayo mahakamani hapo wakati shauri hilo namba 5/2002 lilipokuja kwa ajili ya kutajwa na kushindwa kuendelea kutokana na kukosekana kwa jalada hilo la mirathi lililofunguliwa mika 22 iliyopita na kwamba hadi sasa halijafungwa
Jaji Simfukwe aligoma kuendelea na shauri hilo kwa madai ya kukosekana kwa nyaraka muhimu zenye kuiongoxa mahakama hiyo na kuamua kuahirisha shauri hilo hadi agosti 16 mwaka huu huku akitishia kuifuta kesi hiyo iwapo zitakosekana nyaraka hizo.
Jaji alimwamuru mlalamikaji kupitia wakili wake Stella Simkoko, kuja na nyaraka hizo ikiwemo muhtasari wa uteuzi wa msimamizi wa mirathi, maombi ya uteuzi , barua ya mahakama iliyomteua,orodha ya nali za marehemu na mengineyo.
"Siwezi kuendelea na maombi ya shauri lenu kwa sababu faili lenu halionekani mahakamani,siwezi kutenda Miujiza bila kuwepo kwa nyaraka muhimu ,nendeni mkatafute nyaraka hizo ili kesi yenu iendelee"
Wakili wa mlalamikaji Stella Simkoko kutoka dar es salaam, alisema kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini amesikitishwa jalada hilo kutopatikana pia jalada mbadala lililoagizwa na mahakama hiyo kutengenezwa ili litumike mahakamani hapo pia halikuweza kutengenezwa.
"Mwezi wa tatu tulipata taarifa ya kutoonekana kwa jalada la kesi yetu tulilalamika kwa Msajili wa Mahakama ambaye kupitia barua ya Mei 9 mwaka huu aiikiri kutoonekana kwa jalada hilo na kuniagiza mimi na mteja wangu kutafuta nyaraka za kuunda jalada lingine jambo ambalo hatujaridhika nalo kwa sababu mahakama ndio inapaswa kuwajibika baada ya kupoteza jalada hilo"
"Tumeiomba mahakama itusikilize kwa kutumia vielelezo tulivyokuwa tumewasilisha lakini jaji ametukatalia akiagiza tulete nyaraka muhimu ili aweze kuendelea na shauri letu"
Mmoja ya watoto wa Marehemu, Catherine Kyauka alisema aliamua kufungua shauri hilo ili kuendel2za jalada lililopotea ili mahakama hiyo iweze kutenda haki kutokana na mali nyingi za baba yake kupotea na zingine kugawiwa kinyemela na kuwanufaisha wachache huku baadhi yao watoto wakikosa mgao akiwemo yeye.
Alisema marehemu baba yake , Paul Kyauka Njau alifariki mwaka 2002 na kuacha wajane watatu huku yeye na wenzake 7 wakiwa watoto wa mke wa tatu ambao hawakupata mgao sawa .
Alisema baada ya kifo cha marehemu, kaka yake Emmanuel Kyauka na Frebronia Kyauka walienda mahakamani kufungua kesi ya Mirathi kuomba kuwa wasimamizi wa mirathi huku yeye akiishi nje ya nchi,nchini MAREKANI.
Alisema mahakama iliwateua kuwa wasimamizi wa mirathi mwaka 2003 lakini alisema wasimamizi hao hawakuwahi kukusanya ,kugawa na kufunga mirathi hiyo ila mali nyingi zilipotea kwa kuuzwa na nyingine baadhi ya watoto wakijigawia kinyemela na kujimilikisha kinyume cha sheria.
Catherine aliiomba mahakama kumtendea haki ili aweze kunufaika na mali za marehemu baba yake ambaye aliacha Majumba ya kifahari katikati ya mji wa Moshi,magari ,viwanda na fedha benki.
Alimwomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati kwani anaona kama hatapata haki hasa baada ya kuambiwa jalada limepotea na kuona kwamba anapoteza haki yake.
Shauri hilo la Madai litakuja agost 16 mwaka huu huku baadhi ya wahusika wakiandikiwa wito wa kufika mahakamani wakiwa na nyaraka hizo
Ends..
0 Comments