KESI YA MIRATHI YA TAJIRI KYAUKA YAIVA ,JAJI APOKEA NYARAKA MUHIMU ZILIZOPOTEA ,WALIOTAFUNA MALI ZA MAREHEMU KUZITAPIKA,WARITHI WACHACHAMA MAHAKAMANI TUTAMWONA RAIS SAMIA IWAPO....'

 Na Joseph Ngilisho MOSHI 


MAHAKAMA Kuu ya Moshi Mkoani Kilimanjaro,imeshindwa kuendelea kuzikilizwa kwa shauri la mirathi ya marehemu Paul Kyauka Njau aliyekuwa mfanyabiashara mkubwa mjini Moshi baada ya kukosekana kwa nyaraka mbili muhimu za mwenendo wa shauri hilo.

Kesi hiyo namba 5 ya mwaka 2002, ya mirathi iliyofunguliwa na wasimamizi wa mirathi lakini hadi sasa haikuwahi kufungwa na kusababisha upotevu wa mali za marehemu  inayotokana na wadaawa (walalamikiwa)kujigawia kunyemela.


Jaji wa Mahakama hiyo  Safina Simfukwe alitoa wiki mbili kwa wadaawa, msimamizi wa mirathi Emmanuel  Kyauka pamoja na warithi wengine kuwasilisha mahakamani nyaraka mbili muhimu zilizosalia ili kesi ya msingi iweze kusikilizwa.

Awali Jaji Simfukwe anayesikiliza shauri hilo alidai kupotea kwa nyaraka muhimu zenye kumwongoza katika usikilizaji wa kesi hiyo na kuziomba pande zote zinazovutana kuwasilisha nyaraka walizonazo,ili kesi hiyo iweze kuendelea ,hata hivyo kati ya nyaraka zilizowasilishwa leo ,nyaraka  mbili muhimu ndizo zilizokosekana.

"Ninatoa wiki mbili kuanzia leo agosti 16 hadi Agosti 29 mwaka huu kesi hii itakapo kuja, nyaraka hizo zipatikane ili mahakama iweze kuendelea na usikilizwaji maana kesi hii haihitaji mashahidi ila ni kupitia nyaraka hizo na kusikikiza na baadaye kutoa maamuzi "

Nyaraka zinazohitajika mahakamani hapo ni nyaraka za uteuzi wa msimamizi wa mirathi Emmanuel Kyauka pamoja na orodha ya mali za marehemu (eventory).

Wakili Stella Simkoko anayemwakilisha mleta maombi, Catherine Kyauka  aliishukuru mahakama kwa kupokea baadhi ya nyaraka zinazohitajika ispokuwa hizo mbili ,hivyo wanaimani kesi ya mteja wake itasikikizwa na haki itatendeka.

"Uhakika wa kupatikana kwa nyaraka hizo mbili ni mkubwa zaidi naimani kesi itaanza kusikilizwa  baada ya kupokea baadhi ya nyaraka na mahakama imeagiza warithi wote wenye nyaraka zoOt4 kuhusiana na shauri hilo waziwasilishe mahakamani"

Naye mmoja ya waleta maombi ,Catherine Kyauka alisema anamatumaini makubwa na mahakama hasa baada ya kupokea maombi yao ya kusikikizwa kwa shauri hilo.
"Tumekuwa na matumaini makubwa na  mahakama hasa mara baada ya kupokea nyaraka za mwenendo wa shauri hilo zilizokuwa zimepotea ,mimi binafsi nimepigania haki ya mirathi ya baba yangu kwa miaka 22 ninachoomba ni haki itendeke kuhusu usawa wa mgao wa mali na kama kutakuwa na udanganyifu tutasonga mbele haki haiombwi bali inatafutwa"alisema Catherine. 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi agosti 29 mwaka huu itakapokuja tena kwa ajili ya kutajwa.



Ends..


Post a Comment

0 Comments