Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Kurejea kazini kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda kumeibua faraja kubw kwa wakazi wa Arusha ambao wanaamini Kiongozi huyo ni kimbilio la wanyonge .
Wananchi hao wameenda mbali zaidi kwa kudai mtetezi wao yu hai na wamefarihika kumwona Makonda akiwa na afya njema na kumtaka atimize ndoto yake ya kuwa mbunge wa Arusha mjini ili aweze kuwatetea kwa mapana na marefu .
Wakiongea jana mara baada ya taarifa za ujio wake kusambaa kwa kasi , mmoja ya wananchi hao Emanuel kijuu mkazi wa Ngaramtoni, alisema kutoonekana kwa Makonda na taarifa zilizokuwa zikienea juu ya afya yake zilimfanya augue na kukosa amani .
"Nimefarijika sana baada ya kupata taarifa ya kurejea kwa Makonda kwa kweli Mungu amlinde nilisononeka sana na taarifa zilizokuwa zikienea juu ya kutoweka kwake na maneno mengi yaliyokuwa yakisemwa"
Mwananchi Mwingine Zainab Swalehe mkazi wa Ngarenaro ,alisema kuwa Makonda ni Kiongozi pekee mtetezi wa wanyonge aliyebaki kwa hiyo 'nimefarijika sana kusikia ameonekana tena mungu amlinde na mabaya'
Kurejea kwa makonda imekuwa mwiba mkali kwa wanasiasa waoga ambao wanaamini Makonda atawapokonya jimbo LA ARUSHA mjini ambalo wengi wa wananchi wanatamani agombee ili awe mtetezi wao na uhakika wa kuwatumikia miaka mitano tofauti na ukuu wa mkoa Muda wowote unabadikishwa.
Makonda amerejea ofisini kimyakimya na kuendelea na majukumu yake tofauti na siku alipokuwa akiripoti kwa mara ya kwanza ofisni hapo baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu, kulikuwa na shamra shamra nyingi na mbwembwe za hapa na pale.
Ends..
0 Comments