GAMBO NA WENZAKE WAKALIA KUTI KAVU ,CCM YAWACHOKA NI KUTOKANA NA TABIA ZAO,YASUBIRI MIEZI MICHACHE 'KUWACHINJA' MWENYEKITI WAZAZI TAIFA ASIFU MIRADI YA KIBABE CCM ARUSHA

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa,Fadhili Maganya amesema tabia ya wabunge wa Ccm na viongozi wengine Mkoa wa Arusha kutohudhulia ziara za viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho  bila taarifa yoyote ni dharau na dalili mbaya  kwao kuendelelea na nafasi zao kwani dawa yao ipo jikoni.

Maganya ameyasema hayo leo August 14 ,2024 jijini Arusha ,wakati akihutumia viongozi mbalimbali wa Chama hicho waliojitokeza kumlaki katika ziara yake mkoani hapa ila alichukizwa na kitendo cha wabunge wa mkoa huo akiwemo mbunge mwenyeji, Mrisho Gambo kutoonekana katika mkutano wake wakati taarifa za ujio wake wanazo.

"Chama hiki ni kikubwa kuliko mtu,mbwembwe ,umaarufu ,jeuri na kiburi unazipata kwa sababu unadhamana ya CCM,chama cha mapinduzi kikikuondolea dhamana  your nothing" ,

Alisema kupitia ziara yake wabunge wa ccm walipaswa kuwepo ili kutoa taarifa za utekelezaji wa kazi walizotumwa na chama katika kuwaletea maendeleo wananchi pamoja na changamoto  zilizopo .

"Bila shaka mlijulishwa kuhusu ujio wa Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Taifa ,ila nasikitika siwaoni wabunge hapa ,simwoni mbunge wa hapa (Gambo),simwoni Meya na taarifa bila shaka walikuwa nazo,nilitarajia wawepo hapa kukisemea chama cha mapinduzi, wamsemee Rais ambaye ametoa fedha nyingi za miradi na watueleze wamefanya nini kwa wananchi"

"Sisi viongozi wa chama tunakosa maneno mazuri ya kuwazungumzia ,kumekuwepo ugonjwa kama kidonda ndugu ,naomba mzifikishe salamu zangu kwao,dawa ni fupi tu na ipo jikoni na sisi tumeanza kuhesabu miezi basi ndo salamu hizo"

Aidha Maganya alitoa rai kwa viongozi wa ccm kushikamana kwa pamoja hasa wakati taifa linaelekea kwenye uchaguzi  na kutumia muda huu kutafakari nani anafaa kuwa kiongozi na tupate viongozi bora  na tuhakikishe tunashinda katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.


Alimtaka Mwenyekiti wa ccm Mkoa,  Thomas Sabaya kuondoa makundi ambayo yanaweza kuhatarisha ushindi wetu katika chaguzi zijazo .

Maganya alikipongeza chama hicho mkoani hapa kutokana na uwekezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo na kuzitaka jumuiya zake kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo ili kujipatia vitega uchumi na kuondoa tabia tegemezi.

Alitoa rai kwa chama hicho kuendelea kuwekeza miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa nyumba za watumishi 

Awali Mkuu wa wilaya ya Arusha,Felisician Mtahengerwa alieleza namna serikali ya wilaya inavyoshirikiana vizuri na chama hicho katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Mtahengerwa akiongelea sekta ya utalii Mkoani hapa,alisema imekuwa na mafanikio makubwa baada ya kuzinduliwa  filamu ya Royal Tour kumekuwwpo na idadi kubwa ya watalii kuongezeka huku watalii wapatao 90,000 waliokuwa wafike mkoani hapa wameahirisha kwa kukosa huduma muhimu ikiwemo vitanda vya Malazi ambavyo vimejaa.

Aliwataka wadau wa maendeleo kuwekeza ujenzi wa mahoteli ya kitalii ili kuruhusu ujio wa watalii wwngi zaidi watakao changia kukua kwa uchumi wa mtu moja mmoja na taifa kwa jumla.









Ends..


















Post a Comment

0 Comments