Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Mtaalamu wa Dawa Asili, Kinga na Tiba hapa nchini dokta KAZOBA ametia timu katika viwanja vya Nane Nane Njiro, Arusha ikiwa ni utaratibu wake wa kuhudumia afya za watu kwa kutumia miti shamba na mimea ya asili.
Dokta Kazoba amewataka wananchi kuweza kutumia dawa za asili kama tiba mbadala maana zinauwezo mkubwa wa wa kupambana na magonjwa sugu hasa magonjwa yasiyo ambukiza ambayo kwasasa yanatishia ulimwengu.
Akitoa elimu kwa wananchi katika maonesho hayo ya nane nane wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 30 ya nanenane kanda ya kaskazini Dokta. Kazoba amejinasibu kuwa dawa zake zimefanyiwa utafiti wa hali ya juu na zinauwezo mkubwa wa kupambana na kutibu magonjwa mbalimbali likiwepo tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Amesema kwasasa dunia inasumbuliwa na magonjwa mengi kama vile,kisukari, upungufu wa nguvu za kiume unaotokana na ulaji wa vyakula, magonjwa ya moyo, miguu, ukosefu wa uzazi unatokana na utumiaji wa madawa ya kisasa kwa wanawake, n.k.
"Niwahakikishie watanzania wenzangu nimejikita katika utoaji tiba kwa njia ya asili iliyo boreshwa na dawa zetu zinatoa majibu ya haraka niwaombe wananchi waliyopo Arusha na mikoa jirani wafike katika viwanja hivi vya nanenane njiro nitakuwa hapa kwa siku zote za maonyesho na kuwapa dawa za asili zitakazo tibu maradhi kulingana na maradhi ya mtu".Dokta Kazoba.
Ends..
0 Comments