Na Joseph Ngilisho ARUSHA
KIKAO cha Jumuiya ya maridhiano na amani mkoa wa Arusha,chini ya katibu Mkuu (JMAT)kimeanza maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kitaifa ya maridhiano na amani itakayofanyika mkoani Arusha,mwezi marchi mwakani.
Mkakati huo Umewekwa Augosti 7 mwala huu, kwenye kikao cha jumuiya ya maridhiano na Amani Mkoa cha maandalizi ya siku hiyo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa hoteli ya Golden rose Jijini Arusha.
Kikao hicho kilichofungukiwa na Makamu Mwenyekiti wa JMAT mkoa wa Arusha Sheikh Husein Njunje ,kilichofadhiliwa na benki ya CRDB,kimewashirikisha Viongozi wa dini zote ngazi za kata na kimeteua Kamati ya watu 20 watakaoandaa mkutano huo utakaofanyika marchi mwakani
Mwenyekiti wa kikao hicho Askofu Israel Maasa ,amesema lengo la kikao hicho ilikuwa ni kupata wajumbe wa maandalizi ya kikao kijacho kwa lengo la kuendeleza maandalizi ya mkutano huo mwakani.
Amesema kupitia Jumuiya ya maridhiano na amani hakuna mtu wa dini nyingine anayemuona wa dini nyingine ni adui bali sote ni watu wa familia moja.
Amesema jumuiya ya maridhiano ni chombo ambacho kina Katiba yake ya Jumuiya ya Maridhiano iliyosajiliwa na Jumuiya hiyo ya maridhiano ina Viongozi ngazi ya taifa hadi kata.
Mjumbe wa Kamati kuu ya JMAT Taifa Askofu dkt Eliud Isangya, baads ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa maandalizi amesema kuwa wamekutana kujadili siku ya maridhiano kitaifa itakayofanyika mwezi marchi mwakani Jijini Arusha.
Amesema kuwa wameunda Kamati ya watu 20 lengo ni kuzungumzia amani ,amani ni kitu cha msingi sana katika nchi yetu ambayo imejengwa katika misingi ya amani.
Msingi wa kwanza ni wazee ambao wanatoa amani na mawazo ya utendaji wa kazi unaotendwa na Vijana kwa kuzingatia taratibu wa ngazi zote.
Amesema Vijana wanapaswa kutambua kuwa kupata Elimu sio jambo la lazima kudai haki mbalimbali zikiwemo ajira bali wanapaswa kufuata taratibu .
Amesema vikali vitendo vya ukatilu,ubakaji na unyanyasaji amesema hakuna nchi duniani ambayo haina majaribu kilichopo ni kushirikiana na kuacha mifarakano na hivyo kuondolewa kwa roho yenye tabia chafu.
Amesisitiza mshikamano kati ya Wananchi,Viongozi wa dini na Serikali na vitendo hivyo vya unyanyasaji,ukatili ,ubakaji vitatoweka .
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti,Shekhe Abdulzak Juma, amesema kilichopo ni kuhamasisha Wananchi kuelewa siku hiyo ya maridhiano na amani lengo ni kuleta watu pamoja wakiwemo wanasiasa,Serikali na makundi mbalimbali ya Jamii ili kujenga Umoja na uzalendo.
Amesema amani haipo kwa sababu eti kuna watu wanaipenda bali kuna watu ambao wanaipigania ,hivyo lazima Wadau wawepo ili kudhibiti viashiria wanahitaji Wadau wengi kusimamia amani .
0 Comments