WAMAREKANI WAMCHOKA RAIS BIDEN,WAMTAKA AACHIE NGAZI,YEYE ANG'ANG'ANA KUGOMBEA ANA MIAKA 81

By Ngilisho Tv-MAREKANI 

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatano ameapa kuendelea kuwania muhula wa pili, akipuuza hisia zinazozidi kuongezeka kwamba kushindwa kufanya vizuri katika mdahalo wa kwanza, kutasababisha ajiondowe kwenye kampeni kuelekea uchaguzi wa tarehe 5 Novemba.


“Ninagombea. Mimi ni kiongozi wa chama cha Democratic. Hakuna anayenishurutisha kujiuzulu,” Biden aliwambia washauri wake, kulingana na afisa wa kampeni yake.


Biden na Makamu Rais Kamala Harris walijitokeza gafla katika mkutano wa kamati kuu ya chama cha Democratic kwa njia ya mtandao, wakiutumia kama fursa ya mazungumzo ya kina na kusisitiza umuhimu wa uchaguzi wa 2024.


Biden alisema atasimama tena imara baada ya kuanguka kutokana na kushindwa kufanya vizuri katika mdahalo wa wiki iliyopita.


Uhakikisho wa Biden kwamba atabaki kwenye kinyang’anyiro unajiri huku baadhi ya Wademocrats wakiwa wameanza kuhoji hadharani ikiwa rais huyo mwenye umri wa miaka 81 ana uwezo wa kiakili na kimwili kuendelea na kampeni kali katika kipindi cha miezi minne ijayo, na ikiwa atashinda uchaguzi, anaweza kuongoza nchi katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Post a Comment

0 Comments