Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Taasisi ya dini ya kiislamu ya Twarika Mkoani Arusha imekosoa msimamo wa bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa hatua ya kubariki adhabu ya kufungia wabunge kushiriki vikao vya bunge pale wanaokwenda kinyume na taratibu za bunge ,wakidai utaratibu huo hauna afya na unawanyima haki ya msingi wananchi waliowachagua kuwakilishwa bungeni.
Aidha taasisi hiyo imewasihi wabunge kuacha tabia ya kutoleana maneno makali na kutuhumiana wakati wakichangia hoja mbalimbali bungeni ,badala yake wajikite kuchangia hoja za msingi zenye kuleta tija kwa wananchi.
Wakiongea na vyombo vya habari jijini Arusha ,msemaji wa Twarika Sheikh Haruna Husein,alimpongeza spika wa bunge hilo dktTulia Aksoni kwa kuliongoza bunge hilo kwa uadilifu ila alimwomba kuangalia namna bora zaidi ya kuchukua hatua kwa wabunge wanaokengeuka kuliko adhabu ya kuwasimamisha vikao kwa kuwa adhabu hiyo inalenga kuwaumiza wananchi.
"Hivi karibuni bunge letu limebariki kufungiwa vikao 15 vya bunge, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kwa madai ya kushindwa kuthibitisha tuhuma alizoziibua bungeni ,jambo ambalo linawaumiza wananchi waliomtuma kuwawakilisha "
Kiongozi huyo wa dini alimwomba spika wa bunge hilo nchini,dkt Aksoni kudhibiti vitendo vya wabunge wanaoropoka kwa kutoa kauli chafu dhidi ya wabunge wenzao ama kwa mawaziri hatua ambayo ikiachwa, inafedhehesha bunge .
"Unapompa adhabu Mbunge kutohudhulia vikao kumi na tano vya bunge ina maana unamnyima fursa ya kuwawakilisha mwananchi waliomchagua,tunaomba kwa sheria hii bunge liangalie namna nyingine ya kutoa adhabu"
Katika hatua nyingine Sheikh Haruna amelipongeza bunge hilo kwa kupitisha bajeti ya serikali ya sh,Trilioni 49.34 kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwa ajili ya maendeleo ya watanzania na mustakabalii wa Taifa kwa ujumla.
Pia aliwapongeza viongozi wa serikali akiwemo waziri Mkuu Kasimu Majaliwa walioaminiwa na rais Samia Suluhu Hasani kwa kuendelea kuwatumikia wananchi kwa unyenyekevu jambo ambalo limejenga mahusiano mazuri kati ya wananchi na serikali yao.
Naye Abubakari Kundya , katibu wa kitengo cha habari ,itiladi ,uenezi na mambo ya Nje wa Taasisi ya Twarika na Shaaban Yakob Mwenyekiti Twarika Arusha, walisema wao kama viongozi wa dini wanaipongeza serikali iliyopo madarakani kwa kuendelea kudumisha na kuilinda amani ya nchi yetu kama mboni ya jicho.
"Tuwapongeze viongozi wa dini kwa kushirikiana na serikali katika kuliombea taifa letu kudumisha amani"Alisema Yakob.
Ends..
0 Comments