Joseph Ngilisho,Arusha .
Serikali imewashauri wakandarasi hapa nchini kuanza kutumia teknolojia mpya ya lami baridi katika ujenzi wa miundombinu inayozalishwa hapa nchini na kampuni ya wazawa ya STARPECO LTD inayoonekana kuwa rafiki wa mazingira na sio hatarishi kwa wajenzi.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa afya Dk.Godwin Mollel wakati akikagua mabanda katika mkutano wa tisa wa kimataifa wa ubunifu miundombinu na usafirishaji endelevu Afrika (ICTA) unaofanyika kwa siku mbili jijini Arusha.
Dk. Mollel ambaye alimwakilisha Waziri wa ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kuwa, amefurahishwa na teknolojia hiyo mpya ambayo imeonyesha mafanikio makubwa kwa miundombinu ya hapa nchini ikiwemo unafuu wa gharama na hivyo kuwataka wakandarasi kuchangamkia bidhaa hiyo mpya ambayo haijazoeleka hapa nchini.
"Nimefurahishwa na teknolojia ya bidhaa hii mpya ambayo haijazoeleka sana kwa watanzania ninachowaomba wakandarasi watumie bidhaa hii kuona utofauti kwani inalinda mazingira vizuri na inafanya kazi kama lami moto tuliyoizoea ni vizuri tukawa na matumizi ya bidhaa hii kwenye miundombinu yetu kwani sio hatari hata kuweka majumbani."alisema Dk Mollel.
Naye Meneja masoko wa kampuni ya STARPECO Ltd inayoagiza na kuzalisha lami baridi ,Jones Mkoka amesema kuwa ,kampuni hiyo imekuja na teknolojia mpya ya Lami baridi ambayo inarahisisha ujenzi wa barabara bila kuchemsha lami na hivyo kuwa rafiki wa mazingira .
Mwaka 2014 kampuni hiyo ilianzisha kiwanda kwa ajili ya kutengeneza lami baridi ambapo ina faida kubwa ya utunzaji wa mazingira usalama wa wafanyakazi na napita njia pia kwani .
Ufanyaji kazi kwa haraka hasa katika viraka ila kwa lami baridi fanya hapo kwa hapo haina haja ya kukatakata Korea zege la lami.
Hii sio mpya nchi za Japan,Amerika na ulaya wanafanya kwa kutumia lami.baridi katika ujenzi barabara kubwa kwani inatumia muda mfupi na gharama zake ni ndogo .
"Tunaomba sana Serikali iruhusu matumizi ya lami baridi kwenye miradi yake kwani kwa watu binafsi hasa majumbani sasa hivi wengi wao wanatumia lami baridi katika shughuli mbalimbali kwani inaokoa muda na ni gharama nafuu."amesema.
Hata hivyo amesema changamoto wanayokumbana nayo ni wakandarasi kupangiwa matumizi ya lami moto na kuacha lami baridi katika ujenzi wa miundombinu ya serikali na hivyo kushindwa kutumia bidhaa zao.
Alisema ufanisi wa technologia hiyo ni pamoja na Kuwezesha Kukidhi takwa la Mfuko wa Barabara wa kuziba viraka katika muda wa masaa 48,urahisi wa kufanya kazi na inaokoa muda na gharama.
"Matumizi ya Lami baridi ni kukidhi itifaki za kimataifa katika majezi na ukarabati wa Barabara zetu. Hii itatuwezesha
kulinda mazingira yetu kwa kupunguza adhari za hewa ukaa, joto duniani, matumizi ya miti kulinda Afya za wafanyakazi, hakuna vilipuzi, joto Wala fumes au moshi"
Ends...
0 Comments