Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Wahasibu Barani Afrika (AAAG) utakaofanyika kwa siku tatu katika kituo cha mikutano cha kimataifa AICC jijini Arusha kuanzia Desemba 3 hadi 5 Mwaka huu 2024.
Aidha ukutano huo unatarajiwa kuwakutanisha washiriki wapatao 2,000 kutoka takriban nchi 55 za Bara la Afrika wakiwemo wahasibu kutoka nchini Tanzania.
Mhasibu mkuu wa Serikali,CPA, Leonard Mkude,ameyasema hayo leo Julai 24 Jijini Arusha, wakati alipokuwa akizungumza na Vyombo vya habari akielezea maandalizi ya Mkutano huo ambao utawashirikisha Wakaguzi Wakuu wa hesabu za Serikali barani afrika.
Alisema kuwa lengo la mkutano huo uliandaliwa na Umoja wa Wahasibu Wakuu wa Serikali barani afrika ,AAAG,ni kujenga Imani ya Umma katika mifumo ya usimamizi wa fedha za umma kwa ukuaji endelevu wa uchumi.
Alisema kuwa Mkutano huo utashirikisha Wahasibu,Wakaguzi wa hesabu ,wataalamu wa masuala ya fedha,Tehama ,Vihatarishi na kada nyingine wakiwemo Wahasibu kutoka Sekta binafsi..
Mkude,alisema kuwa Mkutano huo unafanyika kwa mara ya pili tangia kuanzishwa kwake Julai 5 mwaka 2023,ambapo mara ya kwanza ulifanyika Nchini Lesotho February 2024 .
Alisema kuwa Umoja huo ulizinduliwa Mombasa Nchini Kenya Julai 5 mwaka 2023,baada ya Azimio la kufunga Umoja wa Wahasibu waliokuwepo katika kanda mbalimbali wakifanya kazi kwa kutumia lugha za ukanda husika .
CPA,Mkude,alisema,Umoja huo upo chini ya Umoja wa nchi za Afrika,AU,kabla ya kuundwa kulikuwa na Umoja wa Wahasibu wanaozungumza lugha ya Kiarabu,Kiingereza,Kireno,Kifaransa hi yo ilikuwa ni vigumu kuelewana lakini sasa kupitia Umoja huo wamekuwa kitu kimoja
Alizitaja faida za Mkutano huo kuwa ni pamoja na Afrika yenye mafanikio yenye msingi wa ukuaji Jumuishi na maendeleo endelevu ,Bara Jumuishi lililounganishwa kisasa jwa kuzingatia maadili ya Pan-Africanism na maoni ya mwamko wa Afrika na Afrika yenye utawala Bora.
Faida nyingine ni uwepo demokrasia ,kuheshimu haki za binadamu na utawala wa Sheria ,Africa yenye amani na usalama ,Africa yenye utambulisho thabiti wa kitamaduni,urithi wa pamoja maadili na maadili yanauoshirikiwa.
Mkude,alisema kuwa sasa Umoja huo ni chombo kinachowaunganisha Wahasibu wote pamoja barani na kuwa na sauti moja ambapo Benki ya Dunia,Shirika la Global fund Finance, wamejitokeza kusaidia Umoja huo
Mwenyekiti wa Umoja huo wa Wahasibu Wakuu wa Afrika,Malehlohonolo Mahase kutoka Nchini Lesotho, alisema kuwa Mkutano huu unafanyika Nchini kwa ajili ya kujifunza kutokana na Tanzania kuwa kinara katika matumizi ya mifumo ya fedha
Alisema kuwa Tanzania ipo vizuri katika kutekeleza viwango vya kimataifa vya kihasibu, imekuwa ya mfano katika ukuaji wa Uchumi, imeimarika katika suala la ukarimu wa wageni, maendeleo katika teknolojia ya Habari na Mawasiliano na ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi vya utalii hivyo wanachama kuna mambo mengi ya kujifunza.
Alisema kuwa watajifunza zaidi kuhusu fursa za uwekezaji kwenye Utalii na maeneo mengine na Serikali inavyosimamia uchumi pia Nchini kuna demokrasia.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha AICC ,Christine Mwakatobe alisema kuwa ,wamejipanga vyema kuhakikisha wageni wanapokuja wanatoa huduma bora kupitia ukumbi wao wa kisasa .
Aidha amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutangaza nchi yetu duniani kwani hiyo ni kazi kubwa aliyoifanya ya kutangaza utalii kwani wameona mikutano mingi na wawekezaji wanaendelea kuja .
Ends...
0 Comments