TANROADS KUFUNGA CCTV CAMERA NCHI NZIMA KUKABILI UDANGANYIFU KWENYE VITUO VYA MIZANI

Joseph Ngilisho, Arusha .

Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS)  wameanza kufunga kamera (CCTV CAMERA)kwenye Vituo vyake vya  mizani  na kuziunganjsha kwenye mfumo wa serikali kwa lengo la kudhibiti  udanganyifu kwa magari yanayozidisha uzito na kukwepa faini.


Hayo yamesemwa na  Meneja wa mizani TANROADS makao makuu,Injinia Leonard Mombia  wakati akizungumza katika mkutano wa tisa wa kimataifa wa wabunifu miundombinu na usafirishaji endelevu Afrika (ICTA) unaofanyika siku mbili jijini Arusha na kuwahusisha  wakandarasi  kutoka ndani na nje ya nchi.


Mhandisi Mombia alisema kuwa ,tayari hadi sasa  jumla ya vituo 13 zimeshafungwa kamera ikiwa ni mkakati wa kufunga kamera  kwenye vituo vyote vya mizani nchi nzima .   



"Hadi sasa tangia tumeanza zoezi hili vituo vya mizani  13  vimeshafungwa kamera  hizo na   kuunganishwa kwenye mfumo wa serikali.


Alivitania vituo hivyo vya mizani kuw  ni pamoja Mikese,Mikumi,Mpemba,Songwe,Makuyuni.,Njuki,Singida,Nara, Kimokoa,na Vigwaza mkoani Pwani.



Aidha ameongeza kuwa,TANROADS imeamua kuondoa malalamiko ya muda mrefu yanayosababisha msongamano wakati wa kupima uzito kwenye mizani ya kawaida kwa kufunga mizani inayopima gari ikiwa inatembea  (WEIGH IN MOTION (WIM)katika vituo mbalimbali vya mizani.


"Baadhi ya maeneo ambayo  tayari mizani hizo zishamefungwa ni pamoja na Namanga, Vigwaza,Mikese,Mikumi,Wenda,Mpemba,Nara,Rubana na Njuki  na imeonyesha ."Alisema Mombia.



Alifafanua kuwa, hadi sasa TANROADS imefanikiwa kufunga mizani 80 katika mikoa tofauti nchini kwa ajili ya kupima magari yanayozidisha uzito ili kudhibiti uharibifu wa barabara zilizotengezwa na serikali   kwa gharama kubwa. 


Hata hivyo alisema  idadi kubwa ya madereva wamekuwa na uelewa  mkubwa kuhusu matumizi ya barabara kutokana na faini pamoja na elimu inayotolewa na TANROADS.


Ambapo alisema  kiwango cha faini na uzidishwaji wa mizigo umepungua ambapo  kwa mwaka uliopita uzidishwaji wa mzigo ulikuwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka 2020 kiwango cha makosa ya uzisishaji uzito kwa magari  kilifikia wastani wa zaidi ya asilimia 20 .


Hata hivyo Meneja alitoa ushauri kwa wasafirishaji kuzingatia sheria ili kuepuka faini kwenye mizani ,kwani kutofanya hivyo kunasabajisha hasara kubwa kwa serikali pale barabara zinapoharibika na kuzifanyia matengenezo kutokana na ukiukwaji wa  sheria kwa kupakia mizigo mizito kunakofanywa na wasafirishaji wa magari.



Ends...




    


Post a Comment

0 Comments