SHIRIKA LA BIGINIT LAWANOA VIJANA 200 BARANI AFRIKA ,TANZANIA IKINUFAIKA

 Na Tumaini Mafie, Dar es salaam


SHIRIKA la Biginit linalowezesha vijana kujifunza Uongozi wa Jamii na Elimu ya haki Kwa Jamii limewanoa zaidi ya Vijana 200   barani Afrika na Tanzania ikiwa miongoni mwake.


Shirika hilo liliandaa tamasha la siku tatu mkoani Dar es salaamu Kwa lengo la kuwajengea uwezo Vijana wenye shauku ya kuwa viongozi wa Jamii ambapo Kwa mkoa wa Dar es salamu washiriki 60 kutoka Shule tatu za mkoa huo wamepatiwa mafunzo hayo ya Uongozi wa Jamii unaozingatia Usawa na haki  ambapo Moja wapo ya Shule zilizonufaika ni Shule ya Sekondari Temeke.


 Tamasha hilo liliwakutanisha wanafunzi na waalimu katika kushirikishana uzoefu  kupatiwa ujuzi unaohusu Uongozi bora katika jamii, lakini pia vijana waliweza kujifunza namna ya kuanzisha Miradi ya Kijamii na kuiendeleza.





Aidha  Mkurugenzi wa Mradi wa Biginit Elena Tropinova alisema lengo la Mradi huo ni kukuza vipaji vya vijana wenye shahuku ya kuwa viongozi wa Jamii katika bara la Afrika.


"Kupitia warsha, vikao vya elimu, na mikutano ya mfano, washiriki, wanafunzi  na walimu wanaelewa kikamilifu uongozi wa kijamii na jukumu lake muhimu katika kukabiliana na matatizo ya  kimataifa na kwa kawaida kutumia ujuzi na uwezo wa viongozi wa kijamii" alisema Tropinova.


Tropinova alisema   tamasha hilo pia lililenga vijana kuelewa kwanini wanahitajika katika Jamii zinazowazunguka  na umuhimu wa uongozi wa kijamii katika ulimwengu wa leo.

Alisema  mafunzo hayo yanazingatia  mawazo ya mradi wa kijamii kuwezeshwa ambapo  wanafunzi na walimu wanashiriki kikamilifu kukuza ubunifu na uvumbuzi. 


"Mikutano hii huwapa washiriki fursa ya kujifunza kutoka kwa viongozi waliowatangulia  kupata ufahamu na msukumo kwa safari zao wenyewe namna   ya kuongeza kizazi kipya cha viongozi wa kijamii"alisema .


Alisema lengo ni kubadilisha mabadiliko ya mpango wa 2025  ambapo wanatarajia kutoa mafunzo ya uongozi wa kijamii Kwa zaidi ya wanafunzi 200 huku mwaka huu washiriki wakiwa ni 60 tu Kwa Shule tatu za Dar es salaam.


Halikadhalika  Mpango huu, tayari umefanikiwa katika maeneo ya  nje ya Afrika, kama vile Kazakhstan, inalenga mbinu ya ubunifu ya elimu ya ufundi na uongozi wa kijamii ili kuwawezesha viongozi wadogo na waelimishaji. 


Mradi  huo unalenga kutoa mafunzo katika nchi za Tanzania, Nigeria, na Afrika Kusini kwa njia ya vijana wanaohusika na shughuli za kijamii.


Hata hivyo  shirika hili limekuwa likiungwa mkono na Tume ya Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Elimu nchini kugundua mafanikio ya ajabu ya mwanzo katika kuimarisha elimu na ujuzi wa teknolojia kati ya vijana wa Tanzania, kuonyesha ahadi ya pamoja ya kukuza maendeleo ya elimu na teknolojia nchini.


Mwishoooo.

Post a Comment

0 Comments