RC MAKONDA MATATANI ,TUME YA HAKI ZA BINADAMU YAMKUTA NA HATIA YA NZITO ,YAMKALIA KOONI,JAJI ASEMA ALIDHARAU WITO, KITUMBUA CHAKE CHAINGIA MCHANGA HATIMA YAKE BALAA

By Ngilisho Tv  


Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imemkuta Mkuu wa Mkoa wa Arusha (RC), Paul Makonda na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka baada ya Katibu huyo mwenezi wa zamani wa CCM kuagiza mwananchi mmoja kukamatwa na kuwekwa rumande saa 96 bila kufunguliwa mashtaka.

Jaji Mwaimu Mw/kiti  THBUB

Hayo yamesemwa leo ljumaa, Julai 19, 2024 Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa THBUB, Jaji mstaafu Mathew Mwaimu wakati akitoa taarifa ya uchunguzi wa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala bora kwa mwaka 2022/23.


Amesema tume ilipokea malalamiko dhidi ya Makonda katika uchunguzi wa kutoa amri ya kukamatwa na kuwekwa ndani ya mahabusu ya polisi mkazi mmoja wa Arusha (hakutajwa jina). Pia amesema Makonda alipoitwa mbele ya tume kuwasilisha utetezi wake alikaidi


Amesema Tume baada ya uchunguzi imebaini amri iliyotolewa na mkuu wa mkoa haikuwa halali na haikuzingatia aina ya makosa na taratibu ulioainishwa kisheria wa utekelezaji wa mamlaka hayo na kwamba mwananchi huyo hakuwa muhusika wa madai ya msingi, ambayo Makonda aliyatumia ku

Post a Comment

0 Comments