Na Joseph Ngilisho,HAI
WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda ameagiza vyuo vya ufundi nchini kujenga mashirikiano na kampuni kubwa za utengenezaji na kuuza magari ili kusaidia vijana wanaosomea ufundi wa magari kuendana na teknolojia inayokuwa kwa kasi hivi sasa
Profesa Mkenda alitoa agizo hilo mapema leo julai 31,2024 wakati wa halfa ya Uwekaji Jiwe la Msingi Chuo Cha Ufundi Arusha (ATC)Kampasi ya Kikuletwa eneo la Chemka Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.
Alisema ni vema mahusiano yajengwe na kampuni kubwa za magari kama vile Toyota na Mistubishi na kampuni nyinginezo izinazozalisha magari ili kuwezesha vijana kuyajua na kuyatengeneza pale wananchi wanapohitaji matengenezo yake wakati yanapoharibika
Alisema hivi sasa wananchi wananunua magari mengi lakini changamoto kubwa ni jinsi ya kupata mafundi wa kuyatengeneza hivyo endapo mahusiano yakiimarishwa na wanafunzi wanaosomea ufundi wa magari watapngezeka ikiwemo wananchi kutohangaika kutafuta mafundi wa magari yao nje ya nchi.
"Tusifunge milango kwa wataalam wa magari kutoka nje ya nchi waje ili tushirikiane kwa pamoja katika kuhakikisha vijana wetu wa ufundi magari wanapata uwezo zaidi wa kutengeneza magari kwani hivi sasa magari ni mengi yanaagizwa ila wataalam wa kuyatengeneza ni wachache"
Alisema hivi sasa kunachangamoto kubwa katika ufundi wa magari yanayokuja kwa sasa ni mapya na ni manuali na yakuweka gia hivyo lazima tuwe na vijana wengi wanaposoma ufundi wa magari uendane na teknolojia ya magari yanayokuja kwa kasi sana
Alimshukuru Rais Samia Hassan Suluhu kwakutoa fedha nyingi katika sekta ya elimu, ambapo katika mradi huo wa nishati jadilifu katika eneo la Kikuletwa wa Sh bilioni 37.5 ni mradi mmojawapo kati ya miradi minne itakayogharimu zaidi ya Sh.bilioni 187.5 inayotekelezwa na serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia ulishirikisha nchi tatu Kenya, Tanzania na shirikisho la Jamhuri ya Ethiopia.
"Ambapo katika nchi hizi tatu jumla ya miradi hii 16 unatekelezwa ambapo kwa Tanzania tunatekeleza minne ikiwemo huu wa nishati jadilifu uliopo Kikuletwa.
"Lakini pia naagiza nguvu kazi ielekezwe zaidi katika rasilimali ya nguvu kazi ya watu ikiwemo mabweni haya kuendana na uwiano wa wanafunzi watakaokuja kusoma chuoni hapa"
Alisema utekelezwaji wa mradi huo utasaidia nguvu kazi ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa na serikali,katika nguvu za umeme,jua,upepo na tungamotaka na wanafunzi zaidi ya 500 wamepata mafunzo kupitia chuo hicho.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Caroline Nombo alisema kampasi hiyo ya Kikuletwa inajengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia (WB) kupitia mradi wa Afrika Mashariki wa kujengwa ujuzi na uingiliani wa Kikanda (EASTRIP) ambao utaboresha umahiri zaidi katika nishati jadilifu
Alivitaja vituo vingine mbali na hicho cha Kikuletwa vinayotekelezwa nchini ni Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) katika Tehama ,Teknolojia ya Ngozi Mwanza na Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) kinatoa mafunzo ya usafirishaji wa anga na ukikamilika utaongeza fursa kwa wanafunzi kujiajiri na kuajiriwa ndani na nje ya nchi ikiwemo chuo cha ATC.
Alisema kuwa Mradi wa Kujenga na Kuimarisha Ushirikiano wa Kikanda wa Afrika Mashariki(EASTRIP) ni muhimu kwa kuwa una kwenda kusaidia katika utekelezaji wa mabadiliko ya kielimu ambayo yameaanza kutekelezwa kupitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014, Toleo la 2023 pamoja na Mitaala mipya katika ngazi mbalimbali.
Prof. Nombo alisema kuwa 'Mradi huo umeshirikisha nchi tatu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jamhuri ya Kenya na Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia ambazo kwa ujumla zinatekeleza mradi kwa kuanzisha vituo vya umahiri kumi na sita (16).
Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa Mradi wa EASTRIP unatekelezwa kuendana na miradi ya kimkakati ya Kitaifa na umetengewa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 75 sawa na shilingi Bilioni 187.5 kwa ajili ya kuanzisha Vituo vinne vya umahiri nchini katika Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na Chu cha Teknolojia Dar es Salaam ambacho kina Vituo viwili vya Umahiri.
Naye Mkuu wa Wilayani ya Hai Mkoani Kilimanjaro,Amir Mkalipa akimwalisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Nurdin Babu alisema uasisi wa chuo hicho ni mwaka 1933 na leo hii uwepo wa chuo hicho ni historia kwa Tanzania na wananchi wa eneo la Kikuletwa kwani eneo hilo linakubali kilimo pamoja na utalii.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Utawala ya Chuo cha Ufundi Arusha,Kisangire Francise alisema kampasi hiyo ya Kikuletwa imekamilika kwa hatua ya kwanza (phase one) ingawa bado inaendelea kujengwa na alishukuru serikali katika kuhakikisha wataalam wabobezi wanazalishwa kupitia kampasi hiyo
Awali ,Mkuu wa Chuo hicho,Profesa Mussa Chacha alisema uwepo wa chuo hiki kinaongeza umahiri na udahili zaidi katika utoaji wakozi za aina mbalimbimbali zinazotolewa na chuo hico cha ufundi .
.....Ends....
0 Comments