MGODI MAARUFU WA MADINI MERERANI WAUWA WANAFUNZI WAWILI KWA HEWA CHAFU

By Ngilisho Tv


Wanafunzi wawili wa Chuo Kikuu cha Sanyansi na Teknolojia (MUST), wamepoteza maisha baada kuvuta hewa chafu katika mgodi wa machimbo ya madini ya Tanzanite, WA Flanone Mining uliopo katika Mji Mdogo wa Mererani, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara, ambako walikwenda kwa ajili ya mafunzo kwa njia ya vitendo.


Wanafunzi hao waliingia kwenye mgodi huo kwa lengo la kujifunza lakini kutokana na uongozi WA mgodi huo kutochukua tahathali za kiusalama  na kupelekea kupoteza maisha kwa wanafunzi hao.


Kwa mujibu wa Kamanda WA polisi Mkoa wa Manyara , George Katabazi mgodi huo upo  kitalu c ,unaoendeshwa na kampuni ya Franone Mining and Gems LTD na kwamba uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea na mpaka sasa hakuna anayeshikiliwa na polisi kutokana na tukio hilo.


Picha za wanafunzi waliopoteza maisha 

Kamanda aliwataja wanafunzi hao kuwa ni Maulidi Ismail (25) Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Mbeya Mwaka wa pili na Given Enock 23 mwanafunzi wa Mwaka wa kwanza katika Chuo hicho na kwamba wanafunzi hao walienda katika mgodi huo kujifunza elimu ya Miamba.

"Baada ya tukio hilo tumesitisha shughuli za uchimbaji katika mgodi huo ili kufanya uchunguzi zaidi WA tukio hilo"

Jitihada za kuupata uongozi wa mgodi huo ili kuzungumzia tukio hilo bado hazikufanikiwa huku simu ya mmoja ya wakurugenzi wa mgodi huo ikionekana kuwekwa kirusi kwa kuwa muda wote ikipigwa inasema ipo busy !

Picha kwa hisani ya mtandao.

Ends..

Post a Comment

0 Comments