By Ngilisho Tv
Mchungaji wa kanisa la TAG,Ernest George (37), amepandishwa kizimbani na kusomewa shitaka la mauaji ya kukusudia ya dereva, Majuto Seif.
George, ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assembly of God (T.A.G), maarufu Mchungaji George amesomewa shitaka katika kesi ya mauaji namba 19830/2024, leo Jumatano Julai 17, 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza.
Amesomewa shitaka hilo na Wakili wa Serikali, Evance Kaiser mbele ya hakimu, Stella Kiama.
Kaiser amedai mshtakiwa na wenzake wanne ambao hawakuwapo mahakamani walitekeleza mauaji ya dereva huyo Juni 27, 2024 katika eneo la Lugeye wilayani Ilemela, mkoani Mwanza.
Anadaiwa kutenda kosa hilo kinyume cha vifungu vya 196 na 197 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu namba 16 na marejeo ya mwaka 2012.
0 Comments