MASIKINI;RASTA AUAWA KWA FIMBO 70 ZA KIMILA KWA KUTELEKEZA MKE MONDULI,ALIKUWA KAMANDA WA POLISI JAMII KUBOKO CHA VIBAKA ARUSHA

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Kamanda wa Polisi Jamii ,Wille Christopher Maarufu kwa Jina la Rasta Mkazi wa Kwa Giriki Matejoo jijini Arusha ameuawa kwa kuchapwa fimbo 70 za kimila kwa madai ya kutelekeza Mke aliyekuwa akiishi naye wilayani Monduli.


Wille alifuatwa na Ndugu zake alikokuwa akiishi mtaa wa Giriki jijini Arusha siku ya jumatatu Julai 8,2024 na kwenda naye wilayani humo yalipokuwa makazi yake na familia yake, anayodaiwa kuyatelekeza.


Inadaiwa baada ya kufikishwa huko alikalishwa kitako katika kikao cha ukoo na baada ya kuhojiwa alipatikana na hatia ya kuitelekeza familia yake kwa muda mrefu na ndipo kwa mujibu wa mila za kabila la Kimasai iliamuriwa kuchapwa fimbo 70, adhabu ambayo ilitekelezwa .


"Alipofikishwa nyumbani Monduli kikao cha ukoo kilifanyika na marehemu kukutwa na hatia ya kutelekeza familia yake na kuamuriwa kupigwa fimbo sabini, hata hivyo marehemu alishindwa kuhimiri kishindo cha adhabu hiyo na baadaye kufikwa na mauti"kilisema chanzo cha habari


Mmoja ya shuhuda Abdalah Rajabu mkazi wa mtaa wa Giriki, ambaye marehemu alimkabidhi madaraka wakati akielekea Monduli ,alisema siku hiyo marehemu alimfuata akiwa ameongozana na ndugu zake wanne na  kumweleza kuwa anaelekea nyumbani Monduli na angeweza kuchukua siku mbili hadi tatu hivyo alimwomba kukaimu nafasi yake ya ukamanda wa polisi jamii.


"Ni kweli alinifuata akiwa ameongozana na watu wanne na yeye akiwa wa tano akaniambia nimshikie nafasi yake anaenda nyumbani na angeweza kuchukua siku mbili hadi tatu ,lakini chaajabu siku ya jumatatu asubuhi tukapata taarifa kuwa rasta amefariki dunia"


Taarifa zinadai kwamba Rasta alikuwa akiishi kwa Giriki jijini Arusha, ila familia yake akiwemo mke wake alimwacha Monduli lakini hivi karibuni mkewe aliamua  kufungasha virago   na ili atoke nyumbani ilimpasa Mumewe(Marehemu)awepo ili atoe vitu vyake katika nyumba hiyo.


Jitihada za kumpata kamanda wa polisi Mkoani hapa Justine Masejo ili Kuzungumzia tukio hilo iwapo kama kuna watu wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo bado.


End.....












Post a Comment

0 Comments