KIBOKO AUWA MVUVI ZIWA VICTORIA, AMEKUWA AKIUWA MARA KWA MARA ,WANANCHI WALIA NA SERIKALI

By Ngilisho Tv -MWANZA


Mvuvi aliyejulikana kwa jina la Nyiri Katerezi (40), mkazi wa Kijiji cha Nyandago, Kata ya Butondwe, mkoani Geita, amefariki dunia baada ya kushambuliwa na Mnyama aina ya Kiboko katika Ziwa Victoria.

Tukio hilo limetokea wakati marehemu akivua samaki huku wananchi wakiiomba serkali kuumdhibiti Kiboko huyo mwenye mtoto ambaye amekuwa akiua wananchi mara kwa mara katika eneo hilo ambalo wanalitumia kuchota maji pamoja na kufua nguo.

Post a Comment

0 Comments