By Ngilisho Tv KENYA
Inspekta Jenerali wa polisi nchini Kenya amejiuzulu kufuatia wiki kadhaa za maandamano yenye ghasia ambapo zaidi ya watu 40 waliuawa.
Mashirika ya haki za binadamu yameshutumu polisi kwa kuwapiga risasi makumi ya waandamanaji, baadhi yao kuwaua, na kuwateka nyara au kuwakamata mamia kiholela.
Maandamano yalizuka nchini Kenya katikati ya mwezi uliopita kupinga mapendekezo ya nyongeza ya ushuru. Waandamanaji walivamia bunge muda mfupi baada ya wabunge kupitisha mswada huo tata. Hatua ya Rais William Ruto kuiondoa ilifeli kuzima maandamano. Alivunja baraza la mawaziri siku ya Alhamisi .
Kuna mipango ya kuendelea na maandamano ya kuchochea mageuzi.
"MHE. William Samoei Ruto, Ph.D, CGH, Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, tarehe 12 Julai, 2024, amekubali kujiuzulu kwa Eng. Japheth N. Koome, MGH, kama mkuu waPolisi," sehemu ya taarifa hiyo imesema
Share, Mkuu wa Polisi nchini Kenya ajiuzulu
Saa 1 iliyopitaMiili iliyowekwa kwenye mifuko yapatikana eneo la jalalani mjini Nairobi,
.CHANZO CHA PICHA,VIDEOGRAB/TWITTER
Miili iliyowekwa kwenye mifuko yapatikana katika eneo la jalalani karibu na kitongoji duni cha Mukuru Kwa Njenga mjini Nairobi, mtandao wa Capital News umesema.
Wanaharakati waliopata miili hiyo wamebaini kuwa baadhi ya miili imekatwa viungo.
Polisi wamefika kwenye eneo la tukio huku miili zaidi ikiendelea kupatikana.
Haya yanajiri huku mamlaka huru ya Usimamizi wa Polisi (IPOA) ikitoa taarifa na kusema kufikia sasa imepokea malalamishi takriban 10 kuhusiana na visa vya kukamatwa, kutekwa nyara na kupotea kutokana na maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha 2024.
Nane kati ya hayo, IPOA ilisema kuwa waathirika walipatika wakiwa hai, mmoja bado hajulikani alipo huku mmoja akipatikana akiwa amefariki dunia.
IPOA pia ililalamikia ugumu wa kufikia waathirika na hivyo kuwa changamoto kwa wao kuhakikisha uchunguzi wa haraka unafanyika kuhusiana na madai yaliyopokelewa.
0 Comments