Mhe. Balozi Phaustine Kasike akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Bw. Saleh Saad Muhammed.
Mkutano huo ulifanyika kwenye Ofisi za ZIPA zilizopo Maruhubi, Zanzibar ambapo Bw. Muhammed aliuomba Ubalozi wa Tanzania uliopo nchini Msumbiji kuisaidia Ofisi yake kutafuta Wawekezaji kutoka Msumbiji kwa ajili ya kuja kuwekeza Zanzibar.
Aidha, Bw. Muhammed aliuomba Ubalozi kuunganisha Ofisi yake na Taasisi zinazohusika na Uwekezaji nchini Msumbiji ili kuanzisha ushirikiano kwa maslahi ya nchi zetu.
Pamoja na masuala mengine, Mhe. Balozi Kasike aliahidi kuiunganisha ZIPA na Taasisi za Uwekezaji za Msumbiji kama ilivyoombwa na ZIPA.
Aidha, aliushauri Uongozi wa ZIPA kuwasiliana na Uongozi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) ili kujadiliana namna Zanzibar itakavyonufaika baada ya Kituo hicho kusaini Mkataba wa Ushirikiano na Wakala wa Ukuzaji Uwekezaji na Usafirishaji wa Bidhaa za Msumbiji Nje ya nchi (APIEX) wakati wa Ziara ya Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi, iliyofanyika Tanzania hivi karibuni.
Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania - Msumbiji
0 Comments