Na Joseph Ngilisho ARUSHA
FAMILIA zenye watu zaidi ya 20 hazina mahala pa kuishi kufuatia nyumba waliokuwa wakiishi kuvamiwa na kundi la watu na kutolewa nje na kisha nyumba hiyo yenye vyumba 16 kubomolewa.
Akiongea kwa masikitiko mmiliki hiyo iliyopo eneo la Sanawari jijini Arusha, Dickson Mangia alisema watu hao walifika majira ya saa 5 asubuhi na kuwaamuru kutoka nje huku baadhi yao wakipanda juu ya pati na kuanza kungo'a paa na kubomoa nyumba hiyo.
Dickson Mangia
"Tulijaribu kuwahoji watu hao waliokuwa wamebeba sululu,shoka na nyundo,walisema wao wametumwa kutekeleza oda ya mahakama"
Alisema miongoni mwa watu hao alimtambua kiongozi wa kundi hilo aliyemtaja kwa jina moja la MOJAA ambaye ndiye aliyekuwa akitoa amri ya watu wote kutoka ndani ya nyumba huku akisisitiza kuwa hiyo ni amri ya mahakama na aliyekuwa akibisha aliambulia kichapo.
"Tulimwambia atuoneshe notisi ya mahakama inayowapa mamlaka ya kututoa ndani ya nyumba , lakini watu hao waligoma wakisema taarifa ilishatolewa muda mrefu"
Mangia ambaye alijitambulisha kama mmiliki halali wa nyumba hiyo aliyoachiwa kwa maandishi na marehemu bibi yake alikiri kuwepo mgogoro kati yake na mama yake mkubwa aitwaye Anna Philip Moshi ambapo kwa mujibu wa maelezo yake kesi hiyo bado ipo mahakamani.
Wosia.
Alisema watu hao wakati wakitekelez zoezi la kubomoa nyumba hiyo walifanya uharibifu mkubwa ikiwemo kupora baadhi ya mali zao huku mmoja ya wapangaji hao akipoteza sh, laki nne alizokuwa amezihifadhi kwenye kibubu.
"Marehemu bibi yangu alifariki mwaka 1999, nq kabla ya kifo chake aligawa mali kwa watoto wake wote na mimi ndiye nilikuwa naishi naye hapa kwenye nyumba hii na alipoona muda wake wa kuishi duniani umeisha aliniita na kuniandikia karatasi ya kunitambulisha kuwa nyumba hii ni mali yangu,lakini nimeshangaa huyu mama mkubwa ametoka wapi kuja kudai nyumba hii ni mali yake"
Baadhi ya wapangaji waliokumbwa na kadhia hiyo ni pamoja na Alfred John ,aliyepoteza sh,laki nne,Godlizen Kessy na Debora Mkamiki walisema wamepoteza vitu mbalimbali zikiwemo Samani za ndani ambazo ziliharibiwa baada ya kutopewa nafasi ya kutoa vitu nje.
"Mimi nafanya kazi ya kumtembeza mlemavu kwenda kuomba msaada ,ndani lilikuwa na sh, laki nne nilizokuwa nimeziweka kwenye kopo juu ya ukuta, maana huwa nalipwa sh 2000 ila siku nimejikusanya ili nianzishe mtaji lakini ndo hivyo zimepotea kwa sasa sina pa kuishi sijui nitaishije naomba serikali itusaidie ".
Jitihada za kumtafuta kiongozi wa Genge linalodaiwa kubomoa nyumba hiyo aliyetajwa kwa jina moja la MOJAA alikiri kutekeleza zoezi hilo kwa madai kwamba walikuwa wakitekelez amri ya mahakana na kwamba hakuna vitu vilivyoharibiwa wala kuporwa kwani watu wote waliokuwepo walipewa nafasi ya kuondoa vitu vyao kistaarabu.
Ends.
0 Comments