By Ngilisho Tv -BUKOBA
Watuhumiwa tisa wa mauaji ya mtoto mwenye Ualbino Asimwe Novath (2) yaliyotokea mkoani Kagera, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba leo Juni 28, 2024
Asimwe alitekwa Mei 30, 2024 nyumbani kwao katika Kijiji cha Mulamula Wilaya ya Muleba Mkoa wa Kagera na mwili wake ulipatikana Juni 17, 2024 ukiwa umenyofolewa baadhi ya viungo.
Washtakiwa wanaokabiliwa na Shauri hilo ni Elipidius Rwegoshora Mkazi wa Bugandika Wilaya Missenyi aliyetajwa kuwa Mshtakiwa namba moja, Mshtakiwa namba mbili ni Novath Venant Baba wa marehemu (Asimwe), mkazi wa Kata kamachumu Wilaya Muleba. wngine ni Nurdini Amada Masudi, Ramadhani Selestine, Rweyangira Burukadi Alphonce, Dastan Bruchard, Faswiu Athuman kazi (Mganga wa Jadi), Gozbert Alikad na Desdery Everigist kazi wote ni wakazi wa Wilaya Muleba.
Baada ya kutajwa kwa shauri hilo na kusikiliza na Hakimu mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya Bukoba Eliapokea Yona Wilsoni amehailisha kesi hiyo mpaka Julai 12,2024 shauri litakapotajwa tena na washtakiwa wote tisa wamepelekwa Rumqnde Gereza la Bukoba.
0 Comments