HISTORIA YA MAISHA YA DKT SHOGO MLOZI
By Ngilisho Tv
Kuzaliwa:
Dkt Shogo Richard Mlozi alizaliwa tarehe 25 Juni 1979 katika Kijiji cha Bukumbi, Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza akiwa ni binti pekee katika familia ya Prof. Malongo Richard Mlozi na Mwl. Mwanshinga Mlozi.
Sakramenti Takatifu:
• Ubatizo:
Mheshimiwa Dkt. Shogo Mlozi alibatizwa katika Kanisa la Mt. Monica Catholic Parish huko Misungwi, Tanzania.
Komunyo na Kipaimara
Mhe. Dkt. Shogo Mlozi Sedoyeka alipata Komunyo ya kwanza mnamo mwaka 1991 na baadaye Kipaimara katika Kanisa Katoliki la Parokia ya Mt. Maria Imakulata, Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) Mkoani Morogoro, Tanzania.
Ndoa:
Dkt Shogo Mlozi alifunga ndoa Takatifu na Profesa Eliamani Mathew Sedoyeka tarehe 25, septemba 2014 katika kanisa katoliki parokia ya Endasak wilaya ya Hanang' mkoani Manyara na kubarikiwa watoto watano ambao ni Rayan, Unnida, Ulindan, Uiliam na Urbadah.
Pia alipewa ulezi wa mabinti wawili Salidah Sedoyeka na Angela Sedoyeka.
• Elimu ya Msingi
1986 - 1992 Shule ya Msingi Mbuyuni, Mkoani Mwanza.
Elimu ya Sekondari O-level
1993 - 1996 Shule ya Sekondari ya Morogoro mkoa wa Morogoro.
Elimu ya Sekondari ya A-level
1997 - 1999 Shule ya Sekondari ya Kilakala mkoani Morogoro
Elimu ya Chuo Kikuu
Septemba 1999 - Juni 2003 Shahada ya Kwanza ya Uhandisi wa Mawasiliano
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Septemba 2004 - Novemba 2006 Shahada ya Uzamili ya Biashara (MBA)
Masoko ya Utalii kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
2007 - 2011 Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Masoko na Usimamizi wa
Utalii katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia ya Huazhong, Jijini
Wuhan, Nchini China.
2012 - 2013 Mafunzo ya baada ya Shahada ya Uzamivu (Postdoc).
Ujasiriamali na Usimamizi, Shule ya Uchumi ya Hanken, Jiji la Vaasa, Nchini Finland.
Uzoefu wa Kazi:
Uzoefu Mkuu: Alifanya kazi katika ufundishaji, utafiti, na ushauri. Pia aliku-
wa mwanasiasa kama kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hatimaye alichaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
April 2009- Agosti 2017 Mhadhiri Msaidizi, Mhadhiri, Mhadhiri Mkuu na Mkuu wa ldara ya Utalii na Hospitality kutoka Chuo Kikuu cha Tanzania (OUT).
Agosti 2017 - Oktoba 2022 Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Taifa cha Utalii.
Desemba 2022- 2024: Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
Teuzi na Kazi Nyingine:
2018 - 2024 Mjumbe wa kamati ya kitaifa ya kuunda Mwonekano wa Kituo cha Utalii.
2019 - 2024, Mjumbe wa Kikosi Kazi cha Mkakati wa Kuboresha, Kutanua na Kukuza Sekta ya Utalii nchini Tanzania.
2019 - 2024, Mjumbe wa baraza la ujuzi wa utalii nchini Tanzania.
2019 - 2024, Makamu Mwenyekiti na Mjumbe wa Bodi ya Biashara, Utalii na Mipango ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).
Maradhi:
Siku ya Jumamosi tarehe 1 Juni 2024 Mhe. Dkt. Shogo Mlozi Sedoyeka alibarikiwa watoto mapacha wenye afya katika Kliniki Old Arusha kwa njia ya upasuaji.
Siku ya Jumanne, tarehe 11,Juni 2024 Mhe. Dkt. Shogo alianza kulalamika juu ya maumivu makali ya kiungulia, ambapo baada ya kuwasiliana na Daktari wake, alipewa ushauri wa matibabu ya kupunguza tatizo hilo akiwa nyumbani.
Ilipofika siku ya jumatano juni 12, 2024, Dkt Shogo alirejewa tena na tatizo la kiungulia ambapo alipelekwa
kwa matibabu zaidi na kulazwa katika Kliniki ya Old Arusha ambapo baadaye aliruhusiwa baada ya matibabu ya kina na kurudi nyumbani.
Mnamo siku ya Alhamisi, tarehe 13 Juni 2024, wakati wa muda wa asubuhi (saa kumi alfajiri), hali yake ilidhoofika baada ya kuonekana ishara za matatizo ya kupumua.
Alipelekwa haraka hospitalini, lakini kwa bahati mbaya, alifariki akiwa njiani kwenda hospitali.
Chanzo kilichoripotiwa cha kifo ni kiwango cha chini cha oksijeni katika mfumo wa damu.
Hayo ndo maisha ya Dkt Shogo Richard Mlozi hadi kifo chake.
0 Comments