TPHPA YASHAURIWA KUFUNGUA BENK YA KUTUNZIA MBEGU

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


SERIKALI imeishauria mamlaka ya afya ya mimea na Viuatilifu Nchini ( TPHPA) kufungua benki ya kutunzia mbegu za asili za mazao mbalimbali ambazo zipo katika hatari ya kutoweka kwa kuwa ndizo zenye usalama wa chakula.


Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Kilimo,Hussein Bashe ,kupitia hotubabyake iliyosomwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru, Emmanuela Kaganda kwenye ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa kwanza tangia taasisi hiyo ambayo awali zilikuwa mbili ziunganishwe na kuwa ni mamlaka ya afya ya mimea na Viuatilifu ( TPHPA) .


TAASISI hizo zilizounganishwa na kuwa Moja ya TPHPA, ni ile ya huduma ya afya ya mimea iliyokuwa chini ya Idara ya Maendeleo ya mazao Wizara ya Kilimo ( PHS)  na taasisi ya utafiti wa Viuatilifu vya mazao katika ukanda wa kitropiki( TPRI) na kuanzishwa mamlaka Moja ya afya ya mimea na Viuatilifu TPHPA .


Bashe ,alisema kuwa mageuzi makubwa  ya teknolijia  yameleta mabadiliko na kuiwezesha Mamlaka hiyo kutoa gawio la sh, bilioni 3 serikalini na hivyo Serikali itaendelea kujivunia mwelekeo huo ambao unaenda kuwa mkombozi kwa mkulima..


Alisema ili kuleta mageuzi Wizara imeweka vipaumbele ambavyo ni pamoja na kuongeza ajira,kuongeza kasi ya kuimarisha usalama wa chakula,masoko,Ushirika na matumizi ya Tehama kwenye  shughuli za kilimo ambapo  ifikapo mwaka 2030 Kilimo kitachangia asilimia 10%ya Pato la taifa.


Alisema kuwa ifikapo mwaka 2030 Pato linalotokana na kilimo litaongezeka kutoka Dola bilioni 1.5 hadi kufikia Dola bilioni 5 hivyo akaipongeza mamlaka hiyo kwa kuanzisha kitengo cha kuchakata takwimu.


Awali Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka hiyo Profesa Endrew Temu,amesema mwelekeo ni matumizi ya akili mnemba kama njia ya kukabiliana na usumbufu  wa mimea na kutabiri  matokeo ya viuatlifu na visumbufu vya mazao ya Kilimo.


Amesema kuwa  mwelekeo wa bodi hiyo ni kuendelea na majukumu ya kukuza uelewa juu ya afya ya mimea,kuimarisha uwezo ,raslimali watu na Vitendea kazi .


Amesema mkutano huo unatoa fursa ya Wadau na wataalamu kubadilishana uzoefu katika maswala ya kuendeleza kilimo Nchini na msukumo mkubwa ni kuendeleza Vijana kwenye miradi mingi ya kilimo ikiwemo BBT .


Profesa Temu,amesema uwekezaji kwenye teknolijia kufanyiwa biashara  ni mkubwa na utasaidia mkulima kuzalisha kibiashara,na kuwa ukuaji na uwekezaji na matumizi ya mbolea na Viuatilifu .


Amesema teknolijia ya akili mnemba,itawezesha kukabiliana na milipuko ya usumbufu  ya mazao Ndege,panya,nzige ambao wataongezeka  zaidi kutokana na kuongezeka kwa Mashamba na uzalishaj.


Anesema changamoto wanayokabiliana nayo ni kuibuka kwa wadudu waharibifu ,magonjwa mapya ya mazao ambayo yalikuwa hayafahamiki na ongezeko la viumbe wapya  na usugu wa Viuatilifu ,kupitia vinasaba  tofauti na kupunguza katika mimea na kushindwa kuhimili  wadudu hivyo mamlaka inaendelea  kudhibiti na kutafuta  viuatilifu mbadala .


Awali Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya afya ya mimea na Viuatilifu Profesa Joseph Ndunguru,amesema kuwa malengo yake ni kuongeza uzalishaji chakula .


Amesema mkutano huo unatoa fursa  ya kukutana na Wadau ili kutatua changamoto  na kuziboresha ili kuleta  mageuzi ya Kilimo Nchini.

Post a Comment

0 Comments