Tanzania yashiriki kikamilifu Mkutano wa 47 wa Jukwaa la Majadiliano ya Biashara ya Huduma wa Jumuiya ya SADC, Jijini Maputo.
Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Mkutano wa 47 wa Jukwaa la Majadiliano ya Biashara ya Huduma katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa Ngazi ya Wataalam unafanyika jijini Maputo, Msumbiji tarehe 04 hadi 07 Juni, 2024.
Mkutano huo unajadili masuala mbalimbali kuhusu Makubaliano ya Biashara ya Huduma kwa Nchi Wanachama wa SADC yakiwemo; Mapitio ya Taarifa ya Mkutano wa 46 wa Jukwaa la Majadiliano ya Biashara ya Huduma uliofanyika tarehe 09 -11 Novemba, 2023 jijini Cape Town, Afrika Kusini; Kuandaa Mkakati wa Biashara ya Huduma katika Jumuiya ya SADC na Mpango Kazi wake kwa Kipindi cha Miaka Mitano (2025-2029)
Kupokea Taarifa za Hatua za Utekelezaji kutoka Nchi Wanachama kuhusu Ufunguaji wa Sekta za Biashara ya Huduma za Awamu ya Pili; pamoja na kuandaa Taarifa ya Masuala ya Biashara ya Huduma ambayo itajumuishwa kama mojawapo ya Agenda za Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Biashara wa Jumuiya ya SADC.
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo, unaongozwa na Bi. Angelina Bwana, Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.
Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania - Maputo.
05 Juni, 2024
0 Comments