TAÀSISI YA TWARIKA KUTIKISA BARAZA LA IDD ARUSHA,VIONGOZI KADHAA WA SERIKALI KUHUDHULIA,DOTO BITEKO ,RAIS SAMIA ,DC ARUSHA NA MKURUHENZI WA JIJI ARUSHA WATAJWA

 Na Joseph Ngilisho,ARUSHA

Taasisi ya kiislamu ya Twarika Mkoa wa Arusha imeandaa baraza kuu la Idd linalotarajiwa kufanyika siku ya jumatatu makao makuu ya Twarika yaliyopo Matejoo kwa Giriki jijini hapa ambapo pamoja na Mambo mengine watamwombea Dua RAIS SAMIA Suluhu Hasani


Akiongea na vyombo vya habari Mwenyekiti wa Taasisi hiyo mkoa wa Arusha, shabani Jacob alisema baraza hilo la Idd litafanyika kuanzia majira ya saa 8 mchana na  litahudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali akiwemo mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa. 

Aidha alisema miongoni mwa maombi yatakayofanyika siku hiyo ya baraza la Idd ni kuwaombea dua viongozi wakuu wa serikali akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan ili aendelea kudumisha amani katika nchi yetu na kuwaongoza watanzania bila kujali imani na itikadi zao za kisiasa .

Awali msemaji wa Taasisi hiyo ya Twarika,Sheikh Haruna Husein aliwaomba waumini wote wa dini hiyo ,kuonesha mshkamano wa pamoja katika maadhimisho hayo ya baraza la Idd linaloandaliwa na taàsisi hiyo  ya Twarika katika mkoa wa Arusha  

Sheikh Haruna amempongeza Rais Samia Suluhu Hasani kwa kudumisha amani hapa nchini na kupelekea kupata tuzo mbalimbali za heshima.
"Kupitia baraza kuu la Idd sisi kama viongozi wa ngazi za juu tunatarajia kuwa na ajenda muhimu katika baraza hilo ikiwemo kuwaombea dua viongozi wakuu wa serikali na kuwajenga kiimani waislamu kuendelea kuwa wamoja lengonla kushirikiana katika fijra mbalimbali za kimaendeleo"

Sheikh Haruna pia amewapongeza  viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo,Naibu waziri Mkuu dkt Dotto Biteko ,waziri Mkuu Kasimu Majaliwa ,makamu wa Rais Dk Philip  Mpango,mkuu wa Mkoa wa Arusha Paulo Makonda na Mkurugenzi wa jiji la Arusha Eng Juma Hamsin ambao wamekuwa mstari wa mbele kutatua kero za wananchi kwa kushirikiana na vyombo vya dini.




Ends..





Post a Comment

0 Comments