MRITHI WA MREMA TLP HUYU HAPA APATA KURA ZA KISHINDO, SAFU YA USHINDI UCHAGUZI MKUU YANUKIA,LAIZER AHIMIZA MSHIKAMANO

Na Richard Mrusha: Dar es salaam.


Wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) wamemchagua Injinia Aivan Maganza kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho.


Msimamizi wa uchaguzi huo, Rashid Amir, amemtangaza Maganza kuwa mshindi baada ya kupata kura 33.huku wagombea wenzake wanne wakiangukia pua mara baada ya mwanga kishika nafasi ya pili kwa kupata kura 10 huku Stanley kura mbili na wagombea wawili wakipata kura sifuri .




Akizungumza baada ya kuchaguliwa Maganza ameahidi kukibadilisha chama hicho na kuwa cha kisasa huku akituma salamu kwa vyama vingine kwamba vijipange.


“Wale ambao wako TLP kwa nia ya kukivuruga chama au kukikwamisha kuanzia sasa nawatangazia waondoke…nataka nibaki na watu wanaoweza kufanya kazi,” amesema Maganza.


Maganza pia amemteua Riziki Gaga kuwa Katibu Mkuu wa Tlp Taifa baada ya Richard Lyimo kuasi chama  na kuahidi kuunda upya sekretarieti ya chama hicho.


Makamu Mwenyekiti wa Tlp Taifa Dominata Lichungura amesema wamepata wakati mgumu sana kuandaa uchaguzi huo mara baada ya kuandika barua mara mwa mara kwa Msajili wa vyama vya siasa ambaye ni mlenzi wa vyama na baadae kufanikiwa kuitisha uchaguzi ambapo ameomba wajumbe kushikamana kujenga chama hicho ambacho Ayati Mrema amekipigania kwa jasho na damu .


Awali Maganza alikuwa Mwenyekiti wa Vijana TLP Taifa .Maganza Amechukua nafasi ya aliyekua Mwenyekiti wa Tlp Agustino Mrema ambaye alifariki Dunia Jumapili, Agost 21, 2022, saa 12.15 asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.


Na kwa upande wake katibu Mwenezi wa chama hicho Geofray Stephen Laizar amesema ni wakati wa kushikamana kwa pamoja pasipo kuangali dini wala kabila.na kuondoa makundi katika chama hicho .


Amesema baada ya kumpata mwenyekiti mpya chama kitaunda safu ya ushindi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kisha kumsimamisha mgombea urais hapo mwakani 2025 .


Uchaguzi huo umefanyika nchini ya ulinzi mkubwa wa Jeshi la Polisi wakiwa na Silaa mbali mbali kwani hapo mapema  mwaka jana uchaguzi huo uliingia dosari baada ha aliyekua katibu mkuu Richard Lyimo kuarisha uchaguzi gafla wajumbe wakiwa ukumbini tayari kwa uchaguzi mpya wa Mwenyekiti .


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments