Na Joseph Ngilisho- ARUSHA
Katika kikao na viongozi wa wafanyabiashara hao kilichoketi Leo juni 22 Mwaka huu, katika ukumbi wa halmashauri hiyo,Hamsini aliwatoa hofu wafanyabiashara hao kwamba halmashauri hiyo haina nia ya kuwavunjia maduka yao kwa lengo la kuboresha bila kuwepo makubalino ya pande zote jambo lililoibua shangwe.
"Hatuwezi kuvunja maduka bila makubalino ya pande zote hata kama tunania ya kufanya maboresho lazima tufanye vikao vya kuwapatia notisi "
Jana Juni 21 Mwaka huu, majira ya jioni halmashauri hiyo kupitia watendaji wake ilifunga maduka yapatayo 90 ya wafanyabiashara wanadaiwa kodi kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia julai mwaka jana hadi sasa,ikiwa ni njia mojawapo ya kuwashurutisha kulipa madeni yao ili kufukia Marengo ya halmashauri hiyo.
Hata hivyo wafanyabiashara hao kupitia viongozi wao walihamasishana na kufanya mgomo baridi kwa kufunga maduka yao wakiwa na lengo la kutaka suluhu na halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Hamsini alibainisha kwamba kabla ya kuingia mfumo wa TAUSI wafanyabiashara hao wamezalisha deni la sh, milioni 327 ambalo hadi sasa hawajalipa,na baada ya kuingia mfumo wa TAUSI wengi wao pia hawakulipa kodi kabisa na kuzalisha deni la sh, bilioni 1.46 jambo ambalo amesisitiza lazima wafanyabiashara hao walipe kwa asilimia 100 hadi ifikapo juni 30 mwaka huu.
Mhandisi Hamsini ameunda kamati ya Wataalam kwa kuwashirikisha wawakilishi wa wafanyabiashara hao itakayoketi Juni 26 mwaka huu kujadili namna ya kutengeneza mkataba mpya ambao utakuwa na afya kwa pande zote.
Hata hivyo mkurugeni huyo alisisitiz kwamba halmashauri hiuo haina nia ya kuendelea na mgogoro na wafanyabiashara hao na kuwataka wakalipe kodi ya serikali kwa kuchukua control number, wakati mambo mengine yakiendelea.
"Epukeni Radio mbao halmashauri haina nia ya kuvunja maduka yenu hata kama ipo taratibu lazima zifuatwe ikiwemo kuwapatia notisi"Alisema Hamsini na kuibua shangwe kwa wafanyabiashara hao .
Awali miongoni mwa wawakilishi wa wafanyabiashara hao ,Angelus Shokia,David Kileo na Gasto Ngowi walisema kuwa kwa muda mrefu walikuwa wakiomba kupatiwa mkataba mpya ili waendelee kulipa kodi lakini pamoja na barua walizokuwa wakiiandikia halmashauri lakini walikosa majibu.
Wafanyabiashara hao ambao walikiri kutoilipa halmashauri hiyo kwa mwaka mzima ,walisema hatua hiyo ilitokana na msuguano uliokuwepo ila kwa sasa wanamshukuru Mkurugenzi huyo kwa kuwatoa hofu juu ya kuvunjiwa maduka yao na wapo tayari kwa sasa kulipa kodi .
"Ni kweli wengi wetu tunadaiwa madeni makubwa wastani wa sh,250,000 hadi milioni 9 na hii ilitokana na mgogoro wa kutotambuliwa haki zetu ila tunashukuru Mkurugenzi ametuwekea utaratibu mzuri wa kulipa ikiwemo kuingia makubalino kwa wale wanaodaiwa madeni makubwa "alisema Shokia.
Hata hivyo baadhi ya wafanyabiashara hao walienda mbali zaidi na kudai kwamba mgogoro huo unachochewa na baadhi ya wanasiasa wenye maslahi binafsi ambao hapo tayari kuona ukiisha na kumwomba Mkurugenzi huyo kutoa tamko mbele ya baraza la madiwani ili kuwafunga mdomo wanasiasa wanaojinufaisha na mgogoro huo.
Ends...
0 Comments