Na Joseph Ngilisho -Arusha.
Kampuni ya Udalali ya First World Investment Court Broker ya Mkoani Arusha iko katika hatua za mwisho za kukamata mali za kampuni ya The Guardian LTD ya Jijini Dar es Salaam baada ya kampuni hiyo kushindwa kumlipa Mfanyabiashara maarufu wa Madini ya Tanzanite Jijini Arusha ,Justin Nyari kiasi cha shilingi milioni 410 ndani ya siku 14 kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Rufaa.
Kwa mujibu wa nakala ya barua ya Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha,Mariamu Mchomba ya mwezi mei 6 mwaka huu alimwagiza Dalali Allan Mollel kupitia Kampuni yake ya udalali ya First World Investment kuhakikisha anatekeleza amri ya Mahakama ya Rufaa ya kukamata mali za Kampuni ya The Guardin Kama mshitakiwa wa kwanza na mshitakiwa wa pili Kiwanda Cha uchapishaji cha Kampuni ya Printa Afrique .
Baada ya agizo la Naibu Msajili,Mkurugenzi wa First World Investment,Allan Mollel. Mnamo mwezi May 16, 2024 alimwandikia barua Naibu Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha kuwa amefanya kazi ya awali ya utekelezaji wa oda ya Mahakama Rufaa aliyoitoa tarehe 6 May 2024 ya kuupa taarifa uongozi wa Kampuni ya The Guardian juu ya kutakiwa kumlipa Nyari kiasi hicho cha fedha ndani ya siku hizo hata hivyo hajatekeleza hadi muda huo kwisha may 27 mwaka huu.
"Tafadhali rejea amri{Order} ulioitoa may 6 mwaka huu,Utekelezaji wake nikaufanya may 13 mwaka huu kwa kufika kwenye eneo husika ‘’Bulding on Plot no 122 Mikocheni service Trade Area Dar es Salaam in c.t.no 47632 in the name of Guardian limited ‘’
‘’Taratibu za uthamini zinaendelea nitawasilisha taarifa zitakapokuwa tayari na siku 14 za taarifa zitaisha may 27 mwa huu’’ naomba kuwasilisha taarifa ya awali ya utekelezaji kwa hatua zako muhimu’’ ilisema sehemu ya barua ya Mollel
Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya First World Investment Allan Mollel alikiri kutekeleza maagizo ya Mahakama ya Rufaa kwa kampuni ya The Guardian ya kutakiwa kumlipa Nyari shilingi milioni 410 ndani ya muda huo lakini bado mteja hajalipwa kiasi hicho cha fedha.
Ikumbukwe hadi maamuzi haya yamefikiwa ya kushika mali za kampuni hiyo ni baada kesi ilifunguliwa na mfanya biashara huyo wa madini mnamo mwaka 2009 baada ya Gazeti hilo kuchapisha habari za kumchafua Mfanya biashara huyo maarufu na mwanasiasa mkongwe ndipo alipo amua kuliburuza Gazeti hilo mahakamani.
Nyari alikuwa akitetewa Kampuni ya Uwakili ya Loamu Ojare na Kampuni ya The Guardin ilikuwa ikitetewa awali na kampuni ya Ngallo Advocate na kesi hiyo ilifunguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2000 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na Jaji Kakakusola Sambo mwaka 2010 alitoa hukumu The Guardian kumlipa Nyari shilingi milioni 350 lakini Kampuni ya uwakali ya Ngallo Advocate ilikata rufaa Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu hiyo lakini ilishindwa mbele ya Majaji watatu na Mahakama hiyo Mwezi May mwaka huu na kuamuru Nyari kulipwa shilingi milioni 410 pamoja na fidia.
Ends....
0 Comments