MAKAMU WA RAIS DKT MPANGO MGENI RASMI KILELE CHA JUBILEE YA MIAKA 50 YA ECSA, WAKAZI ARUSHA WATAKIWA KUCHANGAMKIA HUDUMA YA AFYA NA MATIBABU BURE

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


Makamu wa Rais,dkt Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, maadhimisho ya jubilee ya Miaka 50 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Mashariki, kati na kusini mwa Afrika inayoshughulikia sayansi ya Afya (Eastern, Central and Southern Africa Health Community, ECSA-HC),yatakayofanyika juni 19,2024 jijini Arusha.

Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Arusha,Frank Mbando alibainisha hayo wakati akiongea na waandishi wa habari katika kongamano hilo la sayansi ya Afya linaloendelea jijini hapa.

Alisema katika Maadhimisho hayo WANANCHI zaidi ya 500 watanufaika na huduma ya kupima na kuchunguza afya zao bure ikiwa ni sehemu ya maadhimisho  hayo , kuchunguza magonjwa yasiyoambukiza kupatiwa tiba.
Frank Mbando
Dkt Omary Chande 




Alisema taasisi ya ECSA ni munganiko wa nchi wanachama  zipatazo 9 na makao Makuu yake yapo jijini Arusha,inaadhimisha miaka 50 tangia kuanzishwa kwake na kilele chake kitafungwa rasmi  juni 19 mwaka huu na dkt Mpango.

Mbando alisema pamoja na  mijadala ya kisayansi inayoendelea kuhusu  tafiti za afya,ECSA iangalie namna ya kujikomboa na kujitegemea zaidi katika sekta ya afya, katika mazingira ya uwezeshaji wa dawa na vifaa tiba ukizingatia kwamba bado nchi za afrika zinategemea zaidi kuagiza vifaa tiba na dawa ambavyo ni gharama kubwa kutoka nje ya nchi zao.

"Juni 19 mwaka huu ndio kilele cha Maadhimisho ya miaka 50 ya jubilee  ya ECSA,tunatarajia dkt Mpango kuwa mgeni rasmi na kwamba kabla ya hapo tutashuhudua kambi ya uchunguzi wa matibabu bure ni vizuri wananchi wakatumia fursa hiyo kuangalia afya zao na  na huduma hiyo inatolewa bure bila malipo"Alisema Mbando.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Yoswa Dambisya alisema kabla ya kilele cha maadhimisho hayo wataalamu wa afya wapatao 250 wamekutana kutoka mataifa mbalimbali kwa lengo kubadilishana uzoefu na kuwasilisha mafanikio ya tafiti mbalimbali za afya.

Dkt Godfrey Sama ambaye ni mmoja ya waandaaji wa Kongamano hilo alisema kilele cha Maadhimisho hayo kitakwenda sanjari na zoezi la uchangiaji damu na pia wanatarajia kutoa huduma ya uchunguzi wa afya kwa watu zaidi ya 500 Katika kambi iliyopo general tyre Arusha.


Naye dkt Omary Chande Kutoka hospitali ya Rufaa Mount ,ambaye alifungua mkutano huo wa kisayansi ya afya. Alisema ulilenga kubadilishana uzoefu na kupata majibu ya tafiti mbalimbali za afya zilizofanywa na wataalamu wa afya kutoka mataifa mbalimbali.

Aliongeza kuwa ujio wa mkutano huo utasaidia nchi ya Tanzania kupata uzoefu wa masuala ya kiafya na namna ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza ambayo kwa sasa bado changamoto ni kubwa hapa nchini 

Kwa upande wake Prof. Tigan Moyo kutoka Zimbabwe amesema kuwa,Wizara za Afya kutoka nchi Mbalimbali zimekuwa zikifanya jitihada kuhakikisha sekta ya afya inaimarika hususani Kwa Usalama wa wananchi hivyo mkutano huo unaangazia mchango wa wataalamu hao katika sekta nzima ya afya .

Mmoja ya wataalamu wa tiba ya afya hapa nchini , dkt Mpoki Ulisubisya alisema kuwa changamoto kubwa iliyopo kwa sasa hapa nchini ni matumizi holela ya dawa bila kufanya vipimo na kusababisha  usugu wa vimelea.Alitoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanafanya vipimo sahihi na kupata dawa sahihi.

Ends....













Post a Comment

0 Comments