MADAKTARI BINGWA NA WAHUDUMU WA AFYA ZAIDI YA 450 WATUA ARUSHA KUTOA MATIBABU BURE ,WANANCHI WAANIKWA KUPATA HUDUMA BURE.

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


MADAKTARI bingwa na wabobezi wa tiba za  magonjwa mbalimbali kutoka hospitali mbalimbali Nchini ikiwemo ,Mhimbili,JKC,MOI, Benjamin mkapa,Milembe,Kcmc,,Aghakhani,Ocean road Mawenzi,Manyara,Mount Meru,Arusha DC,Meru hospitali ya Jeshi Monduli ,wamewasili Jijini Arusha, tayari kwa kambi maalumu ya wiki moja ya kutoa matibabu bure kwa Wananchi..


Akizungumza na Vyombo vya habari leo Juni 22 kwenye uwanja wa mpira wa Sheikh AmriAbeid,mkuu wa mkoa wa Arusha,Paulo Makonda,amesema kuwa maandalizi ya zoezi hilo la kambi hiyo yamekamilika na hivyo anawaombea Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa na mikoa ya jirani wenye magonjwa kuhudhuria kambi hiyo itakayofanyika kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa Sheikh Amri Abeid ,Jijini Arusha.


 Makonda,amesema kuwa maandalizi ya kambi hiyo ya matibabu ya magonjwa mbalimbali ya binadamu itaanza Juni 24 hadi Juni 30 mwaka huu hivyo akawaomba Wananchi wenye magonjwa kuhudhuria na kupata matibabu ya kibingwa na ubobezi  bure 


Amesema kuwa lengo la kampeni  hiyo ni kuwezesha kila Mwananchi anapata huduma ya matibabu ya kibingwa ya ugonjwa unaomsibu.





Amesema anatambua matibabu yana gharama kubwa  na Vipato vya Wananchi vinatofautiana wengine wana uwezo wa kulipiwa boma na wengine hawana .



Makonda,ameyataja baadhi ya magonjwa hayo kuwa ni pamoja na Moyo.Figo.Mifupa,Tezidume,Kisukari,,magonjwa ya akina mama ,Pua,Koromeo,Masikio,ngozi,tumbo,meno.n.k .


Amesema Kampeni hiyo ya matibabu ni mpango wa Rais Samia,wa kuguswa na changamoto za Wananchi hasa wasio na uwezo wa kumdu gharama za matibabu .


Nae Mganga mkuu wa mkoa wa Arusha, dkt Charles Mkombachaka,amesema kuwa yanayoshugukikiwa zaidi ni yadyoambukiza  ikiwemo Kanda na vidoda vya tumbo .


Mkuu wa Mkoa ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wote wa Arusha kujitokeza kwa wingi kwenye Kliniki hiyo, akitoa hakikisho la vipimo, matibabu na dawa bure kwa kila mwananchi atakaebainika na kugundulika kuwa na magonjwa na maradhi ya aina mbalimbali.


"Ndugu zangu asiwaambie mtu, kwenye suala la afya kuna watu wameuza nyumba zao, kuna watu wameuza viwanja, kuna watu wamefilisika biashara zao katika kupambana kuuguza ndugu zao na kuna nyakati nyingine kuna ndugu zetu wameshindwa hata kukomboa miili ya ndugu zao kutokana na madeni ya gharama za matibabu. Neema hii ambayo Mungu ametupa tukaitumie na mikono ya watumishi wa Mungu ikafungue baraka ili tukapate afya kupitia madaktari wetu hawa bingwa." Amesema Mh. Makonda


Kwa mujibu wa Makonda, Hospitali na Taasisi zitakazoshiriki kliniki hiyo ni pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya afya ya akili Milembe, Hospitali ya kanda KCMC, Hospitali ya Kanda Benjamin Mkapa, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Taasisi ya mifupa Moi pamoja na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Mawenzi, SAIFEE pamoja na hospitali na taasisi nyingine za ndani na nje ya Mkoa wa Arusha.

Post a Comment

0 Comments