LINA MIKONONI MWA POLISI,NI MTOTO WA MFANYABIASHARA MAARUFU WA MADINI ARUSHA ANAHOJIWA KWA KUMILIKI MTAMBO WA KUCHAKACHUA POMBE HARAMU,NI HAWARA WA MFANYABIASHARA MKUBWA ARUSHA

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


Mwanamke Lina Raymond Kishumbua Mkazi wa Njiro Jijini Arusha,aliyekuwa akitafutwa na polisi kwa muda Mrefu kwa Makosa ya Kumiliki mtambo wa kuchakachua pombe haramu aina ya Konyagi ,hatimaye amekamatwa na polisi Mkoani hapa.


Lina ambaye ni mtoto wa Mfanyabiashara wa Madini Raymond Kishumbua Mkazi wa PPF jijini Arusha, alikamatwa juzi katika viunga vya polisi baada ya kwenda kituo hapo kufuata gari lake la kifahari lililokuwa likitumiwa na John shayo ambaye pia alikamatwa na polisi kwa tuhuma hizo akiwa  na gari hilo .


Lina anayedaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Shayo alifuata gari hilo baada ya kuhadaiwa  kwamba kesi yake ilikuwa imemalizika na alikuwa hatafutwi.


"Shayo baada ya kesi yake kumalizika mahakamani kwa kutiwa hatiani na kutozwa faini ,alienda polisi kufuata gari hilo ,lakini polisi waligoma kumpatia kwa madai kwamba uminiki unasoma jina la Lina hivyo walimtaka mwenye  gari aende kuchukua ,ndipo Lina akiwa ameongozana na Shayo walifika kituoni hapo na Lina kujikuta matatani akishikikiwa"kilisema chanzo cha habari


Lina ni mshirika wa karibu wa Mfanyabiashara maarufu John Kasian Shayo ambao kwa pamoja wanadaiwa kushirikiana kumiliki mtambo wa kuchakachua pombe feki aina ya Konyagi .


Hata hivyo Shayo anayedaiwa kuwa hawara wa Lina alikamatwa na kufikishwa mahakamani huku Lina akifanikiwa kuwatoroka polisi na kutokomea kusikojulikana.


Shayo alifikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya uhujumu uchumi ambayo kisheria hayakuwa na dhamana na kusota magereza kwa muda mrefu  hadi Juni 11 mwaka huu alikiri makosa na kutiwa hatiani.


Mbele ya hakimu Sheila Manento wa mahakama ya wilaya Arusha,alimhukumu adhabu ya kulipa faini ya sh,520 000 pamoja na kutaifisha gari lake lililokutwa na chupa kadhaa za konyaji feki zilizotengemezwa kinyume cha sheria.


Kwa mujibu wa Wakili aliyekuwa akimtetea Shayo, Moses Mahuna alisema kuwa Mteja wake aliachiwa huru baada ya kukiri makosa na kuingia makubaliano ya kulipa faini ya sh, 520.


"Ni kweli Shayo alikiri makosa na kukubali kuingia makubaliano na mahakama na kulipa sh,520,000 na hivi sasa yupo huru na wala hana mpango wa kukata rufaa ameridhika na maamuzi ya mahakama"alisema Mahuna.


Jana Lina alikuwa akihojiwa katika kituo kikuu cha polisi kutokana na tuhuma zinazomkabili ikiwemo umiliki wa mali yakiwemo magari kubaini iwapo ni zao la uchakachuaji wa pombe haramu ama lah.


Jitihada za kumpata kamanda wa polisi Mkoa Arusha Justine Masejo ili kuzungumzia tukio hilo hazikuweza kufanikiwa.


Ends...







Post a Comment

0 Comments