KISHIMDO MGOMO WA WAFANYABIASHARA ARUSHA,MADUKA ZAIDI YA 1000 YAFUNGWA, VIONGOZI WAO WAKANA KUHUSIKA ,WATISHIA KUJIHUDHULU,MADUKA YENYE MAKABURI STAND NDOGO YAZUA TAHARUKI

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Viongozi wa wafanyabiashara katika jiji la Arusha wamekana kuhusika na mgomo wa wafanyabiashara kufunga maduka na wamewasihi kufungua maduka yao kwa kuwa serikali imeshasikia kilio chao.


Aidha viongozi hao wametishia kuachia ngazi iwapo wafanyabiashara hao wataendelea kukaidi na kutowasikiliza .


Mapema leo maduka zaidi ya1000 katikati ya jiji la Arusha yalifungwa na kusababisha kero kwa wananchi kukosa huduma muhimu za mahitajia jambo ambalo linatishia uchumi wa taifa na vipato vya wananchi.




Akiongea na  vyombo vya habari Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara, Loken Masawe alisema,wao kama viongozi wa wafanyabiashara katika jiji la Arusha hawajui namna mgomo huo ilivyoandaliwa kupitia vipeperushi bila kuwashirikisha.


"Hili linalotokea hapa Arusha sio sawa maana viongozi wetu wapo Dodoma wakijadiliana na serikali ,wanachokifanya wafanyabiashara wamepotoka chamsingi wafungue maduka "


Mwenyekiti kiti huyo alibainisha kilio cha wafanyabiashara hao ni pamoja na kupigwa faini kubwa ya sh,mil.15 kwa wasiotumia mashine za EFDs na kutoa risiti pamoja na utitiri wa Machinga kando ya maduka yao na Malipo ya huduma ya biashara,( Service Levy).


Hatua hiyo imekuja kufuatia mgomo baridi wa wafanyabiashara ambao hadi sasa wamefunga maduka katika maeneo maarufu ya kibiashara eneo la standi kubwa ,standi ndogo ,Makao mapya na baadhi ya maeneo katika kata ya mjini kati na Kaloleni.


Hata hivyo Lokeni ameiomba serikali kusikiliza kilio cha wafanyabiashara hao ili kuepuka hali kama hii kujirudia ikiwa ni pamoja na kutaka suluhu ya pamoja ya kukutana na ngazi ya wafanyabiashara hao. 

"Sisi kama viongozi wa wafanyabiashara tupo tayari kumwaga manyanga kama wafanyabiashara wataendelea kuumizwa na serikali kwa sababu hatutaweza kuvumilia haya yanayotokea, hatuwezi kushuhudia mfanyabiashara anafilisika kwa kukamuliwa na TRA sisi tukiwa kwenye uongozi" 

Aliiomba serikali kuondoa kero zote zinazowasibu wafanyabiashara pamoja na kutazama upya tozo mbalimbali za serikali ikiwepo Kodi.


"Kilichotokea jijini Arusha kinaambukiza kutoka mikoa ya Dar es salaam,Dodoma,Mbeya na Mwanza na Sisi kama viongozi hatupendi kuona hali kama hii ikitokea tunahitaji uchuni wa taifa na mtu mmoja mmoja ukuwe "

Akiongelea changamoto katika eneo la stendi ndogo alisema kunajinamizi lisilojulikana katika maduka hayo yaliyojengwa baada ya kufukuliwa kwa makaburi yakiyokuwepo ndio maana matatizo hayaishi.


Naye katibu wa wafanyabiashara hao Ahmed Nuru alisema hatambui ujio wa mandamano hayo na kueleza kuwa vipeperushi vilivyotumika kuhamasisha wafanyabiashara vimetolewa na watu wasiojulikana.


Hata hivyo alisema wameomba gari la halmashauri kuwatangazia wafanyabiashara kurejea na kuwatangazia wafanyabiashara kufungua maduka yao wakati viongozi wa kitaifa wakiwa makao makuu ya serikali mjini  Dodoma kupata suluhu na serikali juu ya madai yao.


Hatua ya wafanyabiashara kuitisha mgomo baridi na kushindwa kufungua maduka yao kumeibua taharuki kwa wananchi wanaohitaji huduma mbalimbali na kujikuta wasijue la kufanya.



.ends..










Post a Comment

0 Comments