By Ngilisho Tv-Ngorongoro
HALMSHAURI tano kati ya saba za Mkoa wa Arusha zimefanya vizuri katika kutekeleza hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mwaka 2023/24 kwa kupunguza na hoja kuwa chini ya kumi
Pongezi hizo zilitolewa wilayani Ngorongoro Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kutoka nje ya Mkoa wa Arusha,Valence Rutakyamira wakati wa kumalizika kwa hoja za ukaguzi wa katika halmashauri ya saba za mkoa huo
Alisema halmashauri tano zilizofanya vizuri ni pamoja na Longido,Karatu,Meru,Monduli pamoja halmashauri ya Wilaya ya Arusha huku halmashauri ya Jiji la Arusha pamoja na Ngorongoro zikiwa na hoja zaidi 11.
"Kupungua kwa hoja hizo kumepelekea ukaguzi kufanyika vizuri ikiwemo madiwani kuelewa jinsi ya kuzitekeleza huku maofisa maduhuli wa kila halmshauri wakihitahidi kuhakikisha miradi yote inayonunuliwa vifaa inakuwa na nyaraka husika"
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Arusha,Missaile Musa aliagiza halmshauri ya wilaya ya Ngorongoro kuhakikisha magari yaliyokaa muda mrefu bila kutengenezwa ikiwemo ukusanywaji wa mapato ya mauzo ya viwanja zaidi ya sh, milioni 19,568,612 kutoka kwa mwekezaji ambaye hawakumtaja jina lakini bado anadaiwa na halmashuri hiyo kulipa deni hilo kwa halmashauri hiyo ili kuongeza mapato
Ambapo mwekezaji huyo alilipa sh,milioni 5 huku halmashauri ikimdai sh,milioni 14 zilizobaki hali iliyopelekea baraza hilo maalum kuagiza mwekezaji huyo kulipa deni hilo ndani ya siku 90 zijazo ili hoja hoja hiyo ifutike
"Mnahoja zinazoweza kufutwa l hakikisheni mnazifuta na madeni mnayodai yalipwe ili kuondoa hoja 11 kutokea mara kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) 2023/24
Naye Mwekahazina wa halmashauri hiyo,Pascal Mulaji alisema halmashauri hiyo ilikuwa na jumla ya hoja 46 , hoja za zamani zilikuwa 14 ambapo kwa mwaka huu 2023 jumla ya hoja zinaendelea na utekelezwaji hoja 11 .
Mwisho
0 Comments