BUNGE EALA LAPITISHA KWA KISHINDO BAJETI YA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 112.9 2024/25

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki EALA,limepitisha bajeti ya dola za kimarekani milioni 112,984,442 kwa ajili ya matumizi ya jumuiya hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25 ikiwa ni ongezeko la asilimia 9 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka jana 2022/23 iliyokuwa dola 91.6.


Wabunge wa bunge hilo kwa pamoja walipongez bajeti hiyo iliyopendekezwa na sekretarieti ya jumuiya hiyo kutokana na vipaumbele vilivyoainishwa katika kipindi cha 2024/25 wakidai itakuna na manufaa makubwa kwa wananchi wa EAC.


Mbunge wa EALA, Mashaka Ngole kutoka Tanzania alisema bajeti hiyo inatija kwa maendeleo ya wananchi wa nchi wananchama kutokana na  vipaumbele vya bajeti vilivyoainishwa.


"Katika bajeti hii ya 2024/25 yapo mambo ambayo yamepewa kipaumbele ambayo sekretarieti iliyaainisha na sisi kama wabunge tumeridhishwa na bajeti hiyo na tumeipitisha"


Ngole alibainisha baadhi ya vipaumbele, mgao na mikakati ya kuimarisha Uratibu wa Kikanda, ukuaji wa uchumi, na maendeleo ya kijamii katika nchi wanachama wa EAC kwa mwaka wa fedha 2024/2025  .


Hata hivyo alisema ongezeko la bajeti hiyo ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya michango ya wachangiaji kutoka asilimia 57 iliyozoeleka hadi kufikia asilimia 70 ni kutokana na wajibu wa kuchangia kwa nchi zilizokuwa zinasuasua kuwa na mwamko wa uchangiaji.


Naye Mbunge wa Tanzania dkt Abdullah Makame alisema bajeti iliyopitishwa ni nzuri ila haina jipya kwa sababu haitekelezi matakwa na wananchi wa nchi wananchama katika kuwaletea maendeleo kwa asilimia 100.


Alisema jumuiya hiyo imekaa kisiasa zaidi na kuwashauri mawaziri wa EAC kukaa kitako na kufikiria namna bora zaidi ya kuendesha jumuiya hiyo ili iweze kuwanufaisha wananchi wa nchi wanachama.


Dkt Makame  ameonesha wasiwasi namna ya uchangiaji wa michango kwa nchi wanachama kutokana na baadhi ya nchi kusuasua, hatua ambayo alidai kwamba bila michango iliyokamili utekelezaji wa bajeti hiyo utakuwa ni mgumu .


"Miaka yote michango ilikuwa inafikia asilimia 57  ila kwa sasa imefikia asilimia 70 ili kujuia iwe na manufaa lazima michango ifikie asilimia 100 vinginevyo tutaishia matumizi ya kawaida tu"


Kwa upande Katibu Mkuu wa EAC, Veronica Nduva aliwashukuru wabunge wa EALA kwa kupitisha bajeti hiyo na kueleza kuwa atahakikisha anasimamia ipasavyo utekelezaji wa matakwa yote yaliyoainishwa katika bajeti hiyo.


Mchanganuo wa bajeti hiyo ni kama ifuatavyo;Amani na Usalama wa Kikanda: Dola milioni 5.1,Ukuzaji Biashara na Uwekezaji: USD 4.7 milioni ,Maendeleo ya Taasisi: USD 10.4 milioni,Ukuzaji wa Miundombinu ya Sekta Mbalimbali: Dola za Kimarekani milioni 6.2,Kuimarisha Sekta za Kijamii na Uzalishaji: USD 20.3 milioni

,Mashirika na Taasisi za EAC: Dola za Kimarekani milioni 66.3,Mashirika na Taasisi za EAC zilipokea sehemu kubwa zaidi ya bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025, na mgao kama Sekretarieti ya EAC: USD 51,677,120

Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ): USD 4,858,553Bunge la Afrika Mashariki: USD 20,469,040 Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria: USD 7,787,519Baraza la Vyuo Vikuu baina ya Afrika Mashariki: USD 17,287,618 ,Shirika la Uvuvi wa Ziwa Victoria: USD 3,109,586.


Tume ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika Mashariki: USD 2,177,192,Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki: USD 1,641,445,Tume ya Utafiti wa Afya ya Afrika Mashariki: USD 2,451,157,Mamlaka ya Ushindani ya Afrika Mashariki: USD 1,525,212


Hii inafanya jumla ya bajeti iliyotengwa kwa ajili ya vyombo na taasisi kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kufikia dola 112,984,442, ambapo dola 67,785,519 (61%) zitagharamiwa zaidi na michango ya nchi wanachama na mapato mengine ya ndani, na dola 43,936,292 (39%). kufadhiliwa na Washirika wa Maendeleo.




Ends. 













Post a Comment

0 Comments