By Ngilisho Tv
Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga Stephane Aziz Ki ambaye pia ndie mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC kwa msimu uliopita akiwa na magoli (21), ameushukuru uongozi na Mashabiki wa klabu ya Yanga kupitia ukarasa wake wa Instagram. Ameandika;
"Kila kitu kiliwezekana, Asante kwa wachezaji wenzangu, wafanyakazi, kamati ya Raisi na hasa Raisi ,mashabiki, na familia yangu. Pia, nimshukuru Mwenyezi Mungu mara nyingine tena kwa uaminifu wake, msaada wake, uaminifu wake, umenipa mengi msimu mzima"
Kauli hiyo umeleta sito fahamu miongoni mwa mashabiki wa Yanga, baadhi yao wakitafsiri Aziz Ki ndio anaaga kwa maana ya kuondoka ndani ya klabu hiyo, lakini Aziz Ki amekanusa kwa kusema bado yupo sana ndani ya klabu ya Yanga Sc.
0 Comments