WATU 8373 WAHAMA NGORONGORO KWA HIYARI,SERIKALI YAWALIPA MAMILIONI YA ZIADA ,NCAA YAVUKA LENGO LA MAPATO ,KASI YA WATALII USIPIME

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


Serikali kupitia Msemaji Mkuu imesema jumla ya wananchi wapatao 8373 ,sawa na kaya 1,373 waliokuwa wanaishi  katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) tangia kuanza kwa mpango wa uhamaji wa hiari mwaka 2022, wamehama bila kushurutishwa.


Akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha, msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi alisema katika awani ya kwanza iliyoanza juni 16,2022 hadi Januari 17,2023 jumla ya kaya 551 zenye watu 3,010 zilihama .



Alisema mpango huo wa uhamishaji wa hiyari kutoka hifadhi ya Ngorongoro unasimamiwa na wizara ya Maliasili na utalii kupitia Mamlaka ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), huku ujenzi wa makazi Mapya unaratibiwa na Ofisi ya waziri Mkuu(Sera ,Bunge na Uratibu)ikishirikiana na wizara za sekta husika.

Alifafanua kuwa kati yao, kaya 503 zenye watu 2692 zilihamia Msomera na kaya 48 zenye watu 318 na  mifugo  yao ipatayo 15,321 zilihamia maeneo mengine yaliyopangwa.

Matinyi alisema awamu ya pili ilianza Agosti 24,2023 hadi Aprili 28,2023 ambapo kaya 822 zenye watu 5,354 zilihama ,kati yake kaya 745 zenye watu 4,855 ziliende Msomera na 77 zenye watu 489 na idadi ya  mifugo wapatao 21,136 zilihama na wananchi hao kwenda maeneo mengine ya nchi.

Alisisitiza kuwa tangia kuanza kwa mpango huo awamu zote mbili kaya zipatazo 1,373 zenye watu wapatao 8,364 zimeshahama .

Alisema kijiji cha Msomera kimepokea  kaya 1,248 zenye watu  7,547 na walioende maeneo mengine ni Kaya 125 zenye watu 817 huku jumla ya mifugo ipatayo 36,314,ambapo 30,314 ilienda Msomera  na 6,143 ni kwenye maeneo mengine nchini.

Hata hivyo Matinyi alikanusha taarifa kwamba baadhi ya wananchi waliohama kutoka eneo hilo la hifadhi ya Ngorongoro hawajalipwa fidia ama stahili zao na kudai kuwa malipo yote hufanyika mara baada ya wahusika kubomoa maboma yao na kuchagua mali za kuhama nazo tayari kwa safari.

"Wanaohamia Msomera ,Saunyi na Kiteai mbali na malipo ya usafiri na kuhama hulipwa fedha ya ziada sh,milioni 10 na wanaohamia maeneo mengine ya nchi hulipwa ziada ya sh,milioni 15"

Hata hivyo alisema serikali haijasitisha huduma kwa wale ambao bado hawajahama katika eneo hilo la hifadhi ya Ngorongoro, wanaendelea kupatiwa huku utoaji wa elimu nabuhamasishaji kwa wananchi waliobaki ikitolewa .

"Serikali haikasitisha jukumu la kuwahudumia wananchi wake ila kadri wanavyohama baadhi ya huduma zitaendelea kupungua ikiwemo ujenzi wa madarasa"

Wakati huo huo alifafanua kwamba watu waliokuwa wakiishi Msomera katika eneo tengefu bila kufuata utaratibu serikali haikuwaondoa badala yake iliwapati  hati miliki ya kuendelea kuishi katika maeneo hayo na sio kweli kwamba waliondolewa kimabavu licha ya kwamba walikuwa wamevamia maeneo hayo.

Msemaji huyo alisema kuwa mpango wa serikali wa kujenga nyumba 5000,nyumba 2500 zinajengwa katika kijiji cha Msomera, 1500 zinajengwa Kitwana na Saunyi nyumba 1000 huku wakati zaidi ya 100,000 wakitarajiwa kuhamia kutoka hifadhi ya Ngorongoro. 

"Hadi sasa nyumba 1,000 zimekamilika Msomera na kati ya hizo Nyumba 737 zimekamilika zinakaliwa na watu huku nyumba 263 zipo tayari zinasubiri watu wanaohamia"

Katika hatua  Nyingine Matinyi alisema mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeendelea kupolea idadi kubwa ya watalii ambapo kati ya Julai 2023 hadi Aprili 2024 imepokea watalii 780,281 tifauti na mwaka 2022/23 ilipokea wageni 752,000.

Alisema ongezeko la idadi ya watalii  imeenda sanjari na kupanda kwa mapato hadi kufikia sh,bilioni 188.5 na kuvuka lengo la sh,bilioni 155.4.Mafanikio hayo ni kutokana na kuimarisha ulinzi wa rasilimali za wanyama pori wakiwemo faru ambao ni adimu ,kupambana na mimea vamizi,ujangili na kuimarisha nyanda za malisho kwa kudhibiti uvamizi kwa ajili ya wanyama pori 

Ends...








Post a Comment

0 Comments