TANELEC ARUSHA INAVYOCHANGIA UKUAJI SEKTA YA MADINI, WAZIRI MAVUNDE APIGWA MSHANGAO NAMNA TRANSFOMA ZINAVYOUNDWA NA KUSAMBAZWA MIGODINI

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


Kiwanda cha Kuzalisha Transfoma chaTanelec kilichopo jijini Arusha,kimewakaribisha wamiliki wa migodi hapa nchini kutumia bidhaa zake  zinazozalishwa hapa nchini ili kuokoa gharama kubwa ya kuagiza vifaa kama hivyo nje ya nchi ikiwa ni njia moja wapo ya kulinda na kukuza viwanda vya ndani na kukuza uchumi wa Tanzania.

"Tanelec tunafanya ubunifu ili kuisaidia sekta ya madini kukua zaidi na tunatengeneza vifaa vyenye ubora wa hali ya juu na kwa upande wa Transfoma tumebuni  kifaa maalumu cha kulinda mweneno wa umeme  kwa Transfoma kukabiliana na changamoto za umeme na kuifanya idumu muda mrefu"

Hayo yameelezwa na Joseph Tiba  mtaalamu wa vifaa vya umeme Tanelec, wakati akimweleza Waziri wa Madini Anthony Mavunde  alipotembelea  banda lao  katika mkutano wa jukwaa la tatu la utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini, unaofanyika katika ukumbi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Aicc Jijini Arusha.


Tiba alisema Tanelec imekuwa ikijihusisha na utengenezaji wa vifaa vya umeme na watumiaji wakubwa wa vifaa hivyo ni wamiliki wa migodi ya madini jambo ambalo alisema wamerahisisha upatikanaji wa vifaa na kuwaondolea gharama kubwa ya kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi.

Alimweleza waziri Mavunde kuwa pamoja na uzalishaji wa vifaa hivyo ,Tanelec imekuwa ikiendesha mafunzo mbalimbali namna ya kufunga na  kuendesha mitambo ya umeme migodini jambo ambalo limesaidia kuwapunguzia gharama za kuagiz mafundi kutoka nje ya nchi.

"Tanelec imekuwa chachu kwa wamiliki wa migodi kuwawezesha kufikia malengo yao kwa kuzalisha vifaa bora vya umeme kama Transfoma ambazo tunatoa vifaa maalumu kwa ajili ya kulinda usalama wa Transfoma mara kunapotokea changamoto ya umeme "alisema Tiba.

Akiongea katika mkutano huo waziri Mavunde alibainisha kwamba Kampuni  zinazoendesha migodi hapa nchini kwa mwaka jana zimefanya ununuzi wa zaidi ya Trilioni 3.1 kwa kuagiza nje ya nchi vifaa mbalimbali vya mgodini.

Waziri Mavunde ameiagiza Tume ya Madini kumpelekea orodha ya bidhaa zinazoagizwa sana nje nchi ili serikali iwatafute wawekezaji ikiwa ni nia pekee ya kukuza uchuni wa Tanzania.

Ends...

Post a Comment

0 Comments