TAKUKURU YAMSAFISHA MKURUGENZI JIJI LA ARUSHA, UCHUNGUZI WA AWALI RADA ZAKE ZASHINDWA KUNASA ,SASA ANACHAPA KAZI KWA KWENDA MBELE OFISINI

Na JosephNgilisho- Arusha.

Mhandisi Juma Hamsini MKURUGENZI JIJI ARUSHA 

TAASISI ya kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Arusha, imemsafisha Mkurugenzi wa jiji la Arusha Mhandisi Juma Hamsini kwa kumwondoa kwenye tuhuma zilizokuwa zinamkabili baada ya  uchunguzi wa awali kuonesha kwamba hahusiki na tuhuma hizo.

Miongoni mwa tuhuma zilizokuwa zinamkabili yeye na wenzake  ni pamoja  kughushi nyaraka, kuchepusha makusanyo ya Serikali na ubadhirifu wa fedha za umma .

ZAWADI NGAILO ,Kamanda TAKUKURU ARUSHA

Kamanda wa Takukuru Mkoani hapa,Zawadi Ngailo alisema  uchunguzi wa awali uliofanywa na taasisi yake umebaini kuwa mkurugenzi huyo  na mwenzake  hawakubainika kuhusika moja kwa moja na tuhuma hizo zilizoibuliwa na Mfanyabiashara    Wilbard  Chambulo mbele ya mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ambaye aliagiza Takukuru kufanyiakazi tuhuma hizo.

Tuhuma zingime ni kuwepo kwa makampuni hewa, malipo hewa na namba bandia za mlipakodi zilizotumika kuchepusha kodi au mapato yoyote katika halmashauri ya Jiji la Arusha.


Alisema uchunguzi wa awali umebaini watumishi wawili wa halmashauri hiyo wamehusika kughushi nyaraka ikiwamo kutengeneza namba bandia ya mlipakodi na kutumia kampuni hewa kulipia mapato.


Ngailo ameeleza kuwa kutokana na maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda, tayari taasisi hiyo ilikuwa imesha anza uchunguzi wao wa awali toka siku ya kwanza walipo pata malalamiko hayo.


"Maelekezo yalitolewa kwenye kikao kati ya Mkuu wa Mkoa na wafanya biashara wa sekta ya utalii Mkoani Arusha , ofisi yake ilikuwa imeshaanza uchunguzi na uchunguzi huo ulikuwa unahusisha idara ya mapato ( Ushuru wa Huduma ) katika Halmashauri ya Jiji la Arusha". Ameeleza Kamanda Ngailo.

Hata hivyo alisisitiza kuwa bado wanaendelea na uchunguzi na pindi watakapokamilisha wahusika watafikishwa mahakamani.



Takukuru iliingia kazini kutii agizo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kufuatia tuhuma zilizowasilishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (Tato), Wilbard Chambulo akilalamikia kulipa kodi ya huduma Shilingi milioni 24, lakini al8pewa risiti ya Shilingi milioni 3.6 kitu ambacho kilimshangaza.

.....ends....

Post a Comment

0 Comments