SERIKALI KUTUMIA BUNIFU KATIKA MAENDELEO YA TAIFA,MADAWATI NA MAJUKWAA YA SAYANSI ,TEKNOLOJIA NA UBUNIFU YAZINDULIWA ARUSHA

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


SERIKALI itaendelea kuwatambua wabunifu nchini  kwa lengo la kuchagiza maendeleo ya uchumi na kijamii kwa kuzishirisha teknolojia na bunifu ili kukuza uchumi kwakutumia teknolojia zinazoibuliwa sanjari na kuzilinda.

Aidha uwepo wa madawati na majukwaa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yatawezesha bunifu zinazoibuliwa kutambulika ikiwemo bunifu mpya zinazozalishwa katika kata,wilaya na mikoa mbalimbali na kupata fursa za kuongezewa ujuzi zaidi na serikali .

Hayo yalisemwa jana Jijini Arusha Nan Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi n Teknolojia,Dk,Franklin Rwezimula wakati wa uzinduzi na Uanzishwaji wa Madawati na Majukwaa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu .


Dk,Rwezimula alisema katika kuhakikisha bunifu zinakuzwa serikali imeendeleza  bunifu 283  zilizobuniwa na watanzania ,huku bunifu 42 kati ya hizo zimeingia sokoni .

Serikali imeendelea kuweka mazingira  wezeshi kwaajiliya uendelezaji wa vituo ambapo hadi sasa vituo 75 vya umahiri na ubunifu vimeshwa ambapo hadi sasa Tanzania  inavituo 12 vya umahiri vya kilimo,mifugo,afya ,nishati na tehama ili kuibuni bunifu zinazozalishwa kwenye sekta isiyo rasmi

Alisema pia kongani 21 zimeanzishwa kwaajili ya kutoa fursa zinazoshabihiana ikiwemo kubadilishana uzoefu katika nyanja za ubunifu Kwa wajasiriamali nchini.

"Wabunifu wengine huwezi kuwakuta shuleni wapo mitaani hivyo mafunzo haya Kwa maofisa elimu kata,maendeleo ya jamii yanalengo kuwajengea uwezo kwaajili ya kuendeleza bunifu maeneo ya serikali,hivyo lazima tuwainue wabunifu wengi chini na bunifu zao ziweze kuwainua kiuchumi"

Alisema wadau wakuu ni Tume ya Sayansi na Teknolojia,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia pamoja na Costec na kuongeza kuwa majukwaa ya bunifu yanaanzishwa katika shule zote ikiwemo vyuo vya ualimu, sanjari na madawati ya sayansi na bunifu kuanzia shule za msingi.

Alisema awamu ya kwanza ya mafunzo hayo yameanza katika mikoa ya Arusha,Tanga na Dar es Salaam ambao yatasaidia wanafunzi kuibua bunifu zao katika shule mbalimbali na kuongeza kuwa suala la sayansi, teknolojia na ubunifu liwe ni ajenda katika maeneo mbalimbali ikiwemo dawati mahususi katika maeneo mbalimbimbali ili yawe kiungo katika vyanzo vyote vya sayansi na teknolojia.


"Lazima tuanze kupanda mbegu kwa wanafunzi wetu mashuleni kupitia sayansi na bunifu ili na sisi tuwe na wabunifu wengi zaidi nchini lengo ni kuhakikisha kunakuwa na tathimini ya kueleweka ya masuala ya bunifu sanjari na kuwaibua wabunifu na wagunduzi wa matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu"

Huku Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais,(Tamisemi) anayeshugulikia Elimu ya Awali na Msingi,Susan Nussu  aliwataka maofisa elimu kata kuhakikisha wanaibua vipaji vya wabunifu kwenye kata zao ili kuhakikisha matokeo mazuri ya bunifu yanajulikana na kuleta matokeo tarajiwa katika kukuza vipaji

Naye Ofisa Elimu Mkoa wa Arusha,Abel Mtupwa akimwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Arusha,Missaile Musa  alisema maofisa elimu na walimu wanadeni kubwa la kulipa serikali Kwa kuhakikisha wanafaulisha vema wanafunzi kwakua serikali imewekeza miundombinu mizuri katika sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa shule mbalimbali nchini.





Ends..

Post a Comment

0 Comments