Na Joseph Ngilisho, Arusha
Aidha Makonda ameagiza kusimamishwa kazi kwa wahusika wote waliotajwa na tuhuma za rushwa . JHU
Akiongea na wadau wa utalii katika kikao kilichofanyika Mkoani hapa, Makonda pia alimwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Missaile Mussa kuwasimamisha kazi watumishi wote waliotajwa kuhusika na tuhuma hizo ili kupisha uchunguzi.
Makonda mechukua hatua hizo baada ya Mwenyekiti wa waongoza watalii mkoa wa Arusha Wilbard John Chambulo kulalamika mbele yake akidai kuwa baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji hilo wamekuwa wakitengeneza nyaraka bandia pamoja na kuchepusha baadhi ya makusanyo ya kodi zinazotokana na sekta ya Utalii.
Awali Chambulo katika mkutano huo alihoji kwanini apewe risiti tofauti za kulipa kodi zenye namba tofauti za kampuni yake na kuongeza kuwa hayupo tayari kulipa kodi kwenye namba tofauti za malipo kwa Jiji la Arusha na hatakuwa Mwenyekiti wa kikao kilichotakiwa kukaa na Rc awali bali awepo Mwenyekiti mwingine wa muda wa Tato ili kibaini mahesabu kama yapo sahihi ili walipe kodiAlisema halmashauri ya jiji la Arusha imedai kuwa alilipa kodi ya sh ,milioni sh,milioni 24 kwenye kodi (service Levy) aliyokuwa akidaiwa lakini akashangazwa kuona taarifa za malipo alizopatiwa zikionyesha kuwa amelipa milioni tatu (3) pekee hivyo kuibua hisia hasi na madai ya uhujumu wa fedha za umma kwa baadhi ya maofisa Jiji hilo.
Chambulo alidai Watumishi hao wamekuwa na makampuni hewa ya utalii pamoja na kuwa na namba tofauti za ulipaji wa kodi na usajili hewa wa makampuni yenye kufanana na makampuni halisi ya utalii yalipo ndani ya Jiji la Arusha.
Alisema si jambo la busara kwa mfanyabiashara kulalamikia jambo hilo na kisha yeye kutoa maagizo kama Rc wa Arusha kuwa Mkurugenzi, Juma Hamsini kushughulikia jambo hilo kwa kuunda timu ili kubaini ukweli wa madai ya Chambulo lakini cha ajabu badala ya mkurugenzi Hamsini kuunda tume maalum na kumpa ripoti Rc Makonda akakimbilia kwenye vyombo vya habari
"Sasa naagiza Takukuru kuchunguza sakata hili na watakaochunguza hao maofisa wanaokusanya kodi wasikanyage ofisini hadi hapo watakapobainika kuwa hawana makosa na wewe Mkurugenzi Hamsini wasaidie Takukuru kutoa nyaraka unazodai kuwa Chambulo anakwepa kodi ili kujua ukweli wa tukio hili"Alisema Makonda
Mhandisi Juma Hamsini ,Ded ArushaAwali Aprili 15,2024 Halmashauri hiyo imekanusha vikali madai hayo ya Chambulo ambaye ni mfanyabiashara na mdau wa masuala ya utalii wa muda mrefu kuwa si ya kweli baada ya kuibua tuhuma hizo na kudai halmashauri hiyo ilifanya ufuatiliiaji wa taarifa za mifumo ya kikodi za Chambulo (kwa kuwa hakuna fedha inayopokelewa mkononi), na baada ya ufuatiliaji huo walijiridhisha masuala kadha wa kadha yanayoleta utata kwenye ulipaji wa kodi za serikali hususan zile anazopaswa kulipa kwenye halmashauri hiyo
Mhandisi Hamsini alisema inadaiwa kuwa Chambulo anamiliki kampuni mbili tofauti ambazo ni 'The Tanganyika Wilderness Camps Limited' na 'Tanganyika Wilderness Camps Limited' ambazo kampuni zote hizo licha ya kwamba zinafanya shughuli zake kwenye maeneo mbalimbali lakini usajili wake umefanyika Arusha, lakini namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) inayotumika ni moja jambo ambalo linaleta majibu kuwa mmiliki wa kampuni hizo ni mtu mmoja ambaye ni Chambulo
Mara baada ya malalamiko hayo Makonda alisema serikali yake inawajibikaji kuwa mlezi wa wafanyabiashara na wawekezaji wa mkoa wa Arusha na hivyo kamwe hatovumilia mtendaji yeyote anayekuwa sababu ya kukua kwa vitendo vya rushwa na kuua biashara zilizopo mkoani Arusha.
Aidha Makonda amepiga marufuku kwa Halmashauri zilizopo mkoani Arusha kutumia Polisi kwenda kudai kodi kwa wafanyabiashara na kuagiza zitumike teknolojia zaidi kwenye kukumbusha na kudai madai mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Arusha.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amelazimika kuahirisha kikao kazi hicho na kuagiza kupangwa kwa tarehe nyingine chini ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha ili kupata muda mzuri wa kujadiliana na kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazokwamisha ukuaji na ustawi wa sekta ya Utalii mkoani Arusha
MKuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha Zawadi Ngajilo alisema wamepokea maagizo hayo na wameshaanza kuyafanyia kazi ikiwemo kuwahoji watuhumiwa.
"Tumepokea maagizo ya mkuu wa Mkoa na yunayafanyia kazi mara moja na tukikamilisha tutawasilisha taarifa kwake Kwa hatua zaidi.
Chombo hiki cha habari kilimtafuta Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Mhandisi Juma Hamsini baada ya kuzagaa kwa taarifa kwamba amekamatwa na Takukuru yeye na watumishi wenzake kuhusiana na tuhuma za Rushwa,ambapo alisema yeye yupo huru na hajakamatwa na yupo Mkoani Dodoma.
"Mimi nipo huru nipo Dodoma na sijakamatwa, hizo taarifa nizawapi hizo tuhuma zinazosemwa mimi sikuwepo Arusha wakati hayo yakitokea "
Ends......
0 Comments